Putin: Kadhia ya Hijab mashuleni itatuliwe kisheria nchini Russia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i21076-putin_kadhia_ya_hijab_mashuleni_itatuliwe_kisheria_nchini_russia
Rais Vladimir Putin wa Raussia amesema kuwa, masuala yote yanayohusiana na vazi la staha ya wanafunzi wa kike Waislamu yaani Hijab katika shule za nchi hiyo, inabidi yatatuliwe kwa njia za kisheria.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Dec 09, 2016 04:20 UTC
  • Waislamu wa Russia
    Waislamu wa Russia

Rais Vladimir Putin wa Raussia amesema kuwa, masuala yote yanayohusiana na vazi la staha ya wanafunzi wa kike Waislamu yaani Hijab katika shule za nchi hiyo, inabidi yatatuliwe kwa njia za kisheria.

Televisheni ya Rusia al Yaum imeripoti habari hiyo na kumnukuu rais Vladimir Putin akisema jana kwamba, suala la sare na mavazi katika skuli za Russia lina umuhimu mkubwa na inabidi litatuliwe kwa mujibu wa sheria.

Amesema, katika nchi nyingi za Ulaya kumepigwa marufuku Hijabu mashuleni lakini inabidi kuzingatia kuwa Waislamu nao wana haki na inabidi haki za watu binafsi zisivunjwe hivyo kuna wajibu wa kufanyika uchunguzi zaidi na kuangalia ni kitu gani kinaweza kufanyika kuhusiana na suala hilo.

Rais Vladimir Putin wa Russia

 

Rais wa Russia ameongeza kuwa, nchi yake ni ya kisekulari lakini inaheshimu imani na itikadi za dini zote na inabidi watu wote walizingatie hilo.