Putin: Ukraine na washirika wake wamegeukia kwenye ugaidi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i138050-putin_ukraine_na_washirika_wake_wamegeukia_kwenye_ugaidi
Rais wa Russia amesema: Vikosi vya jeshi la Ukraine na washirika wake haviwezi kuzuia kusonga mbele kwa jeshi la nchi hii na vinapoteza maeneo zaidi kila siku, kwa hivyo vinageukia ugaidi.
(last modified 2026-04-29T09:59:02+00:00 )
Apr 29, 2026 09:54 UTC
  • Rais Vladimir Putin wa Russia
    Rais Vladimir Putin wa Russia

Rais wa Russia amesema: Vikosi vya jeshi la Ukraine na washirika wake haviwezi kuzuia kusonga mbele kwa jeshi la nchi hii na vinapoteza maeneo zaidi kila siku, kwa hivyo vinageukia ugaidi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la   Sputnik, Vladimir Putin amesema katika mkutano wa Bunge la Russia siku ya Jumanne kwamba: "Tunajua kuwa utawala wa Kiev na washirika wake wameamua kutumia njia za kigaidi. Sababu za jambo hili ziko wazi kwa kila mtu: adui hana uwezo wa kuzuia kusonga mbele kwa askari wetu kwenye mstari wa mbele. Wanapoteza maeneo kila siku."

Putin ameongeza kuwa: "Kwa msingi huu, Kiev imeamua kufanya ugaidi dhidi ya malengo ya kijeshi na ya kiraia. Wanatumai kwamba hatua hizi zitabadilisha hali ya mambo. Hatua hizi hazitabadilisha lolote,

Rais wa Russia ameonya kuwa shambulizi la hivi majuzi la ndege zisizo na rubani za Ukraine kwenye kiwanda cha kusafisha mafuta cha Tuapse huenda likasababisha madhara makubwa ya kimazingira.

Hapo awali, kamanda wa jeshi la Ukraine, Alexander Sirsky, alikiri kwamba jeshi la Russia limezidisha operesheni zake za kijeshi na kwamba hali ni ngumu kwa jeshi la Ukraine.