Dec 17, 2016 04:23 UTC
  • Vifo vinavyotokana na utumiaji mihadarati na pombe Marekani vimeongezeka mara tatu

Watafiti wa elimu ya tiba nchini Marekani wametangaza kuwa uchunguzi waliofanya katika maeneo 3,100 ya nchi hiyo unaonesha kuwa tangu mwaka 1980 hadi sasa idadi ya Wamarekani wanaofariki kutokana na utumiaji madawa ya kulevya, pombe na maradhi yanayotokana na matatizo ya akili imeongezeka mara tatu.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na taasisi ya "Tathmini ya Vipimo vya Uzima" ya Chuo Kikuu cha Washington, tangu mwaka 1980 hadi sasa, idadi ya Wamarekani wanaofariki kutokana na utumiaji mihadarati na maradhi yanayotokana na matatizo ya akili katika majimbo ya Kentucky, Virginia Magharibi na Ohio imeongezeka kwa asilimia 200.

Unga wa mihadarati

Utafiti huo aidha umeonyesha kuwa kuna visababishi vingine vingi vya vifo vipatavyo 21 ikiwemo ugonjwa wa kisukari, maradhi kama Ukimwi na Kifua Kikuu pamoja na vifo vinavyosababishwa na ajali za barabarani.../

Tags