Waislamu wa Rohingya wanakabiliwa na hali mbaya
Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa Waislamu wanaotaabika wa Rohingya wanaendelea kuishi katika hali ya kutisha licha ya ahadi zilizotolewa na chama cha upinzani cha nchi hiyo kilichoshinda uchaguzi kuwa kitalinda na kutetea haki za waliowachache huko Myanmar.
John Ging Mkurugenzi wa Oparesheni katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa Inayohusika na Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (UNOCHA) ameyamesema hayo baada ya kuutembelea mkoa wa Rakhine ambako Waislamu wa kabila la Rohingya wamekuwa wakikabiliwa na mashambulizi ya Mabudha ukiwemo ukandamizaji.
Waislamu wa Rohingya wasiopungua 140,000 wanaishi makambini baada ya vijiji vyao kuchomwa moto mwaka 2012.
Ging amesema alishtushwa kuona makazi hayo ya muda wananakoishi Waislamu wa Rohingya, ambayo baadhi yanakaribia kuanguka. Amesema kuwa Waislamu wengi wa Rohingya hawapatiwi huduma za tiba kwa sababu tu ya dini yao.