Feb 09, 2017 07:18 UTC
  • Ubelgiji: Saudia inaeneza fikra za Uwahabi barani Ulaya

Ubelgiji imeeleza wasi wasi wake juu ya kuenea kwa kasi mwangwi wa Uwahabi katika nchi hiyo na kote bara Ulaya kwa ujumla.

Uchunguzi uliofanywa na Kituo cha Taifa cha Kushughulikia Migogoro OCAM umebainsisha kuwa, Uwahabi unaenea kwa kasi kubwa katika aghalabu ya misikiti nchini humo, kwa kutumia pesa, ufadhili na uungaji mkono wa serikali ya Riyadh.

Ripoti ya uchunguzi huo iliyochapishwa na gazeti la De Standaard la Ubelgiji inaonyesha kuwa, mbali na kuwamwagia fedha Maimamu wa misikiti hiyo inayoeneza fikra za Kiwahabi, utawala wa Aal-Saud umekuwa ukitoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi kwenda kusoma nchini Saudi Arabia, ambapo huwa wanafunzwa fikra na idiolojia za Kiwahabi.

Kuenea utakfiri na Uwahabi barani Ulaya

Uchunguzi wa kituo cha OCAM umesema kuwa, Ubelgiji ni miongoni mwa nchi zenye idadi ya juu ya watu wenye fikra za Kiwahabi barani Ulaya, wanaoenda Iraq na Syria kujiunga na magenge ya kigaidi kila uchao. 

Viongozi wa Ubelgiji wanasisitizia umuhimu wa kuchukuliwa hatua za maana kwa ajili ya kukabiliana na suala zima la kupenya makundi hayo yaliyopotea hususan Uwahabi na wanachama wake wa kigaidi wa Daesh katika nchi hiyo na bara Ulaya kwa ujumla.

Sio vibaya kukumbusha hapa kuwa, Oktoba mwaka jana 2016, wanaharakati wa kutetea haki za binadamu waliandamana mbele ya ubalozi wa Saudi Arabia huko Brussels mji mkuu wa Ubelgiji kulalamikia na kupinga jinai za utawala wa Aal Saud.

Tags