Wamarekani wengi wanapinga sera za Trump dhidi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i28784-wamarekani_wengi_wanapinga_sera_za_trump_dhidi_ya_iran
Uchunguzi wa maoni uliofanyika hivi karibuni umeonyesha kuwa zaidi ya asilimia 40 ya Wamarekani wanapinga sera za Rais Donald Trump wa nchi hiyo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
May 07, 2017 23:04 UTC
  • Wamarekani wengi wanapinga sera za Trump dhidi ya Iran

Uchunguzi wa maoni uliofanyika hivi karibuni umeonyesha kuwa zaidi ya asilimia 40 ya Wamarekani wanapinga sera za Rais Donald Trump wa nchi hiyo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Uchunguzi huo wa maoni uliofanywa na Televisheni ya Fox News umebaini kuwa, asilimia 44 ya raia wa Marekani hawaafiki hata kidogo sera za Trump dhidi ya Iran.

Aidha uchunguzi huo unaonyesha kuwa asilimi 43 wanaunga mkono sera za Trump dhidi ya Iran huku asilimia 13 ya walioshiriki katika uchunguzi huo wa maoni wakisema hawana la kusema kuhusu suala hilo.

Kwa kuzingatia kupita siku 100 tokea Trump achukue hatamu za utawala Marekani, kukosekana muelekeo wa wazi wa sera za kitaifa na kimataifa ni jambo linaloashiria kuchanganyikiwa wakuu wa serikali mpya ya Marekani.

Wapinzani wa sera za Trump

Ni wazi kuwa sera zilizo dhidi ya Iran za watawala wa Marekani hazina uungaji mkono wa umma katika nchi hiyo. Matokeo ya uchunguzi huo wa maoni yalitangazwa kwa mara ya kwanza Aprili 27.