Donald Trump, Mohammad Bin Salman ni watu hatari zaidi duniani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i29050-donald_trump_mohammad_bin_salman_ni_watu_hatari_zaidi_duniani
Gazeti la Independent la Uingereza limeandika kuwa, Rais Donald Trump wa Marekani na Mohamad bin Salman, Naibu Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia ni watu wawili hatari zaidi duniani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 13, 2017 23:00 UTC
  • Donald Trump, Mohammad Bin Salman ni watu hatari zaidi duniani

Gazeti la Independent la Uingereza limeandika kuwa, Rais Donald Trump wa Marekani na Mohamad bin Salman, Naibu Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia ni watu wawili hatari zaidi duniani.

Katika makala iliyochapishwa katika toleo la Jumamosi la Independent, waliowengi duniani wanaamini kuwa, Trump ndiye mtu hatari zaidi katika sayari ya dunia na wiki ijayo ataelekea Saudi Arabia. Akiwa Riyadh, kati ya wengine, atakutana na Mohammad Bin Salman Naibu Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi anayetajwa kushika namba mbili kama mtu hatari zaidi duniani.

Gazeti hilo limeandika kuwa, Mohammad Bin Salman mwenye umri wa miaka 31 kimsingi ndiye anayetawala Saudia kwani baba yake, Mfalme Salman mwenye umri wa miaka 81 anaugua na hana uwezo wa kusimamia ufalme huo. Katika kipindi cha miaka miwili na nusu tokea ashike wadhifa wa waziri wa ulinzi, amekuwa akichukua maamuzi mabaya na hatari kwa sababu hana uzoefu na wala hakubali ushauri wa busara.

Mfalme Salman wa Saudi Arabia

Independent limeandika kuwa,  Mohammad Bin Salman mbali na kuingilia mambo ya ndani ya Syria alianzisha vita dhidi ya Yemen mwaka 2015 vita ambavyo vingali vinaendelea huku watu karibu 13,000  wakiwa wamepoteza maisha. Aidha Wayemen milioni 17 wanakabiliwa na baa la njaa kutokana na hujuma hiyo ya Saudia. Gazeti hilo limeandika kuwa, Trump na Mohammad bin Salman ni watu wawili wasiojali na wala hawatafakari kuhusu natija ya vitendo vyao na kwa msingi huo ushirikiano wa watu hao wawili ni tishio kwa eneo la Mashariki ya Kati ambalo linakumbwa na misukosuko mingi zaidi duniani.