UN yaituhumu Ukraine kuwa inatuma silaha Sudan Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/world-i29110-un_yaituhumu_ukraine_kuwa_inatuma_silaha_sudan_kusini
Umoja wa Mataifa umeituhumu Ukraine kuwa imekiuka vikwazo vya kimataifa dhidi ya Sudan Kusini kwa kuiuzia nchi hiyo ya Afrika silaha.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
May 15, 2017 07:32 UTC
  • UN yaituhumu Ukraine kuwa inatuma silaha Sudan Kusini

Umoja wa Mataifa umeituhumu Ukraine kuwa imekiuka vikwazo vya kimataifa dhidi ya Sudan Kusini kwa kuiuzia nchi hiyo ya Afrika silaha.

Taarifa ya Timu ya Wataalamu wa Umoja wa Mataifa imesema silaha hizo za Ukraine zimekuwa zikitumiwa na pande zote hasimu nchini Sudan Kusini.

Imesema ndege aina ya Ilyunshinil-76 ya Ukraine iliyoondoka katika uwanja wa ndege wa Kharkiv nchin humo na kuelekea Uganda mnamo Januari 27, ilikuwa imesheheni silaha mbalimbali, zikiwemo ndege ndogo za kivita aina ya L-39, ambazo hatimaye ziliwasili Sudan Kusini.

Silaha mbalimbali zikiwemo bunduki

Inaarifiwa kuwa, Ukraine iliipa tenda kampuni moja ya Ushelisheli ya kuiuzia silaha Wizara ya Usalama wa Ndani ya Sudan Kusini ambazo zimekuwa zikiingizwa Juba kupitia Sudan na Uganda.

Hivi karibuni, ripoti nyingine ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa ilibainisha kwamba, silaha zinazoingia nchini Sudani Kusini zikitokea Ulaya na Israel zimekua zikipitia nchini Uganda na Senegal na kwamba zimekua zikipewa serikali pamoja na upinzani.