Trump atuhumiwa kuzuia uchunguzi wa FBI
https://parstoday.ir/sw/news/world-i29204-trump_atuhumiwa_kuzuia_uchunguzi_wa_fbi
Rais Donald Trump wa Marekani anatuhumiwa kujaribu kuzuia uchunguzi wa Idara ya Upelelezi ya nchi hiyo FBI kuhusiana na faili lililozua utata na mjadala mkubwa nchini humo kuhusiana na madai ya uagiliaji wa Russia katika uchaguzi wa rais wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 17, 2017 09:04 UTC
  • Trump atuhumiwa kuzuia uchunguzi wa FBI

Rais Donald Trump wa Marekani anatuhumiwa kujaribu kuzuia uchunguzi wa Idara ya Upelelezi ya nchi hiyo FBI kuhusiana na faili lililozua utata na mjadala mkubwa nchini humo kuhusiana na madai ya uagiliaji wa Russia katika uchaguzi wa rais wa nchi hiyo.

Siku moja tu baada ya vyombo vya habari kufichua kwamba Doland Trump aliwapa Warussia habari za siri za Marekani, gazeti la New York Times la nchi hiyo limeandika kuwa Trump alimtaka James Comey, mkuu wa zamani wa idara hiyo kusimamisha uchunguzi kuhusiana na mazungumzo yaliyofanyika kati ya Michael Flynn, Mshauri wa zamani Usalama wa Taifa wa Marekani na Warussia. Limeendelea kusema kuwa hatua ya Comey ya kukataa kutekeleza amri hiyo ya Trump huenda ndiyo iliyompelekea rais huyo kumfuta kazi ghafla. Isitoshe inasemekana kuwa Trump pia alimtaka Comey atangaze wazi na bila ya masharti yoyote utiifu wake kwake jambo ambalo lilipingwa vikali na mkuu huyo wa zamani wa idara ya FBI. Bila ya kujali sababu iliyopelekea kufutwa kazi afisa mkuu huyo wa FBI sasa ni wazi miongoni mwa vyombo vya habari na fikra za waliowengi nchini Marekani kwamba Rais Donald Trump alimfuta kazi afisa huyo kutokana na uchunguzi muhimu aliokuwa ameuanzisha kuhusiana na tuhuma za uingiliaji wa Warussia katika uchauguzi mkuu wa rais wa nchi hiyo.

James Comey na Trump

Hata hivyo Trump na washauri wake wa karibu wanasema kuwa suala la kuajiri na kuwafuta kazi viongozi wa ngazi za juu wa nchi hiyo ni katika madaraka aliyopewa rais wa nchi hiyo na kwa hivyo watu hawapasi kulalamikia hatua yake hiyo. Licha ya hayo inapasa kufahamika wazi kwamba kuna tofauti kubwa katika suala zima la kufutwa kazi James Comey na maafisa wengine wa ngazi yake waliofutwa kazi huko nyuma kwa sababu Comey alifukuzwa kazi kwa madhumuni ya kupotosha na kufunika uchunguzi muhimu na nyeti aliokuwa ameuanzisha dhidi ya utawala wa Trump. Wakati huohuo hatua ya Trump kumfuta kazi Comey ni pigo kubwa kwa heshima na hadhi ya Kogresi ya nchi hiyo iliyokuwa imetaka uchunguzi wa kina ufanyike katika faili la uhusiano wa Trump na Russia. Katika upande wa pili, madai ya viongozi na taasisi za kisheria za Marekani zimeanzisha mjadala mkubwa nchini humo kuhusiana na kashfa ya Rais Trump kuwapa Warussia habari za siri za Marekani.

Michael Fylinn, Mshauri wa zamani wa Usalama wa Taifa wa Marekani

Lakini katika kujibu mapigo ya wakosoaji wake, Trump amesema kupitia ujumbe mfupi wa Twitter kwamba ni haki yake ya kisheria akiwa rais wa nchi hiyo kukutana na kubadilishana mawazo na habari na viongozi wa nchi nyingine. Hata hivyo wapinzani wake kutoka vyama vyote viwili vya Republican na Democrat wanasema kuwa hana haki yoyote ya kuwapa viongozi wa kigeni, na hasa Wairi wa Mambo ya Nje wa Russia, habari za siri kubwa za Marekani. Na hasa ikitiliwa maanani kuwa inasemeka kuwa Marekani ilipata habari hizo za siri ya juu kutoka kwa maafisa wa utawala ghasibu wa Israel, jambo ambalo huenda likatatiza pakubwa uhusiano wa pande mbili hizo.

Kwa vyovyote vile kila wakati unapozidi kupita ndivyo kashfa mpya za habari za siri na kiusalama katika utawala wa Trump zinavyozidi kufichuka. Katika wiki za mwanzo za kuingia madarakani Trump huko White house, ni maafisa wa timu yake ya uchaguzi tu ndio waliokuwa wakituhumiwa kushirikiana na Warussia katika kuathiri mkondo wa uchaguzi wa rais wa Marekani.

Congress ya Marekani

Lakini hivi sasa mshale ulio na makali wa tuhuma za kutolewa habari za siri kubwa  kwa Russia na kufanya juhudi za kuzuia uchunguzi wa polisi ya FPI pamoja na kumtisha mkuu wa zamani wa idara hiyo ya upelelezi umeelekezwa moja kwa moja kwa Trump mwenyewe. Kila moja ya tuhuma ambazo hivi sasa zinaelekezwa kwa Rais Trump ina uwezo wa kumfanya ashtakiwe mahakamani na kusailiwa bungeni. Hata hivyo hakuna dalili yoyote ya kuwepo juhudi kama hizo za ima kumshtaki mahakamani au kumsaili bungeni rais huyo mwenye utata mkubwa. Pamoja na hayo haijulikani ni kwa kiwango gani Trump ana uwezo wa kuendelea kuvumilia wimbi hilo kali la ukosoaji na mashinikizo ya vyombo vya habari na wapinzani wake katika Kongresi na jamii ya wanahabari za siri nchini Marekani.