UNHCR: Mamilioni ya watu wamekuwa wakimbizi duniani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i30684-unhcr_mamilioni_ya_watu_wamekuwa_wakimbizi_duniani
Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa (UNHCR) imetangaza kuwa, watu milioni 65 na laki sita walikuwa wakimbizi kote duniani hadi kufikia mwishoni mwa mwaka uliopita wa 2016.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 19, 2017 10:58 UTC
  • UNHCR: Mamilioni ya watu wamekuwa wakimbizi duniani

Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa (UNHCR) imetangaza kuwa, watu milioni 65 na laki sita walikuwa wakimbizi kote duniani hadi kufikia mwishoni mwa mwaka uliopita wa 2016.

Taarifa iliyotolewa na UNHCR imesema kuwa, vita, ukatili na unyanyasaji unaoendelea katika nchi zenye migogoro kama Sudan Kusini, umewalazimisha watu milioni 65 na laki sita kuwa wakimbizi hadi mwishoni mwa mwaka 2016.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, idadi hiyo inaonesha ongezeko la watu laki tatu ikilinganishwa na mwaka wa kabla yake wa 2015. 

UNHCR: Idadi ya wakimbizi inaongezeka duniani

Mkuu wa Mamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa, Filippo Grandi amesema kuwa, hicho ndicho kiwango cha juu kabisa cha wakimbizi tangu kuanza kusajili idadi ya wakimbizi. Amesema ongezeko hilo lisilo na kifani linaonesha kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2016 mtu mmoja kati ya kila 113 duniani alikuwa mkimbizi na kwamba nusu yao wana umri wa chini ya miaka 18.

Sudan Kusini inatambuliwa kuwa na kasi kubwa zaidi ya watu kuwa wakimbizi na kwamba inahitajia msaada wa dharura.