Jeshi la Iran liko tayari kukabiliana na adui yeyote
https://parstoday.ir/sw/news/world-i34767-jeshi_la_iran_liko_tayari_kukabiliana_na_adui_yeyote
Naibu Kamanda wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema jeshi hilo liko tayari kukabiliana na chokochoko za adui yeyeote dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 24, 2017 01:06 UTC
  • Jeshi la Iran liko tayari kukabiliana na adui yeyote

Naibu Kamanda wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema jeshi hilo liko tayari kukabiliana na chokochoko za adui yeyeote dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Akizungumza Jumamosi, Brigedia Jenerali Ahmad Ridha Pourdastan alisema: "Tunafuatilia kwa karibu vitisho vya maadui na wakati huo huo kuimarisha uwezo wa Jeshi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran."

Aidha amesema Jeshi la Iran linaendelea kuwa tayari kukabiliana na kundi la kigaidi la ISIS nchini Iraq, Syria au eneo lololote lile.

Ameongeza kuwa Jeshi la Iran limefanya mazoezi mbali mbali kwa ajili ya kuimarisha uwezo wa kukabiliana na adui. Brigedia Jenerali Pourdastan amesema njama zote za maadui dhidi ya Iran zimegonga mwamba hadi sasa kutokana na uwezo wa jeshi shupavu la majini na pia ushujaa wa majeshi ya anga na nchi kavu.

Kombora la Balistiki la Emad la Iran ambalo limeundwa na wataalamu Wairani

Kamanda huyo wa ngazi za juu amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina uwezo wa kuunda silaha inazohitaji na pia kuonyesha uwezo wake wa kijeshi katika maji ya kimataifa kama vile Bahari ya Hindi. Wakati huo huo siku ya Jumamosi Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Amir Hatami alisema Iran haitaomba ruhusa kwa yeyote katika kuimarisha uwezo wake wa kijeshi. Amesema madamu baadhi ya maadui wanaendelea kutoa vitisho dhidi ya Iran, nchi hii itazidi kujiimarisha kijeshi.

Iran inasisitiza mara kwa mara kuwa uwezo wake mkubwa wa kijeshi si tishio kwa nchi zingine bali sera yake ya kimsingi ya kijeshi ni kujihami na kumzuia adui kuhujumu.