Antonio Guterres: Makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yanapaswa kuheshimiwa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA kwa kifupi, yanapaswa kulindwa na kutekelezwa na kuongeza kuwa, makubaliano hayo ya kimataifa ni muhimu na ya lazima kwa ajili ya kulinda usalama na uthabiti wa dunia.
Antonio Guterres amesema hayo jana na kusisitiza kwamba, kuuna udharura kwa makubaliano hayo ya nyuklia kudumishwa. Hii si mara ya kwanza kwa Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa kuunga mkono na kusisitiza juu ya udharura wa kutekelezwa makubaliano hayo ya nyuklia yaliyofikiwa kati yya Iran na kundi la 5+1 linaloundwa na nchi za Russia, China, Marekkani, Uufaransa, Uingereza pamoja na Ujerumani.
Aidha Federica Mogherini, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya juzi alisisitiza kwamba, kuna ulazima wa makubaliano hayyo yya nyukllia ya JCPOA kuheshimiwa na kueleza kwamba, makubaliano hayo ya kimataifa yamewaletea ushindi wananchi wa Iran na ulimwengu kwa ujumla.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, Iran haitayachana makubaliano ya nyuklia ya JCPOA maadamu upande wa pili haujayachana, lakini kama upande huo utayachana, basi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itayararua vipande vipande makubaliano hayo.
Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, aliyasema hayo jana alipoonana na mamia ya vijana wenye vipawa na vipaji bora vya kielimu nchini Iran na kuongeza kuwa: Nchi za Ulaya zimesimama pamoja kupinga vitisho vya Rais wa Marekani vya kutaka kuyachana makubliano ya JCPOA kutokana na kuwa zinaelewa kwamba makubaliano hayo yana manufaa kwao na kwa Wamarekani na kusisitiza kuwa, msimamo huo wa nchi za Ulaya ni mzuri, lakini hautoshi.