Uchunguzi: Wamarekani wengi wanamtambua Trump kuwa ni "mpumbavu"
Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanyika nchini Marekani yanaonesha kuwa, neno "mbumbavu" ndilo linaloingia katika bongo na fikra za Wamarekani wengi baada ya kusikia jina la Rais wa nchi hiyo, Donald Trump.
Idadi kubwa zaidi ya watu walioshiriki katika uchunguzi huo wa maoni uliosimamiwa na Chuo Kikuu cha Quinnipiac wamesema kuwa, neno la kwanza kabisa linaloingia akilini mwao baada tu ya kusikia jina la Donald Trump ni "mpumbavu".
Matokeo ya uchunguzi huo wa maoni yanaonesha kuwa, asilimia 53 ya walioshiriki wanaamini neno la kwanza linalopaswa kutumiwa kwa ajili ya kumuarifisha Rais wa Marekani, Donald Trump ni "mpumbavu", asilimia 44 wanasema ni "kidhabi na muongo" na asilimia 36 wanasema ni "baradhuli".
Maneno 30 kati ya 48 yalliyochaguliwa kwa ajili ya kumuarifisha Donald Trump katika uchunguzi huo wa maoni yalikuwa hasi dhidi ya kiongozi huyo wa Marekani.
Uchunguzi huo wa maoni umeonyesha kuwa, asilimia 57 ya Wamarekani hawaridhishwi na utendaji wa Trump.
Uchunguzi huo umefanyika katika siku za kati ya tarehe 6 hadi 11 Disemba na kuwashirikisha Wamarekani elfu moja 211.