Waislamu Marekani waandamana dhidi ya uamuzi wa Trump kuhusu Quds
https://parstoday.ir/sw/news/world-i37721-waislamu_marekani_waandamana_dhidi_ya_uamuzi_wa_trump_kuhusu_quds
Maelfu ya Waislamu wa Marekani wamefanya maandamano wakipinga hatua ya Rais wa nchi hiyo, Donald Trump ya kuitambua rasmi Quds kuwa ni mji mkuu wa utawala haramu wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 17, 2017 08:44 UTC
  • Waislamu Marekani waandamana dhidi ya uamuzi wa Trump kuhusu Quds

Maelfu ya Waislamu wa Marekani wamefanya maandamano wakipinga hatua ya Rais wa nchi hiyo, Donald Trump ya kuitambua rasmi Quds kuwa ni mji mkuu wa utawala haramu wa Israel.

Katika maandamano hayo yaliyoitishwa na Baraza la Jumuiya za Kiislamu nchini Marekani kuelekea kwenye Kongresi ya nchi hiyo washiriki walipiga nara na kaulimbiu zinazowatetea na kuwaunga mkono watu wa Palestina. 

Waandamanaji hao Wamarekani pia walikuwa na bendera za Palestina na mabango yenye maandishi: "Trump na Netanyahu ni sawa na kurejea Manazi", na "Quds ni mji mkuu wa Palestina."

Waislamu wa Marekani waandamana kupinga sera za Trump

Miongoni mwa shakhsia walioshiriki katika maandamano hayo ya kupinga uamuzi wa Donald Trump wa kuitangza Quds inayokaliwa kwa mabavu kuwa ni mji mkuu wa Israel ni mwandishi wa Kiyahudi, Miko Peled, kasisi maarufu anayepinga vita, Medea Benjamin na Imamu wa Msikiti wa Islamu mjini New York, Abdul Alim Musa.

Tarehe 6 mwezi huu wa Disemba Rais Donald Trump wa Marekani aliitoa tangazo la kuitambua rasmi Quds tukufu na Kibla cha Kwanza cha Waislamu kuwa ni mji mkuu wa utawala haramu wa Israel licha ya upinzani mkubwa wa jamii ya kimataifa.