Kongamano la kuwapinga Wazayuni wa Israel lafanyika nchini Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i41127-kongamano_la_kuwapinga_wazayuni_wa_israel_lafanyika_nchini_marekani
Jarida la Washington Report kwa kushirikiana na kitengo cha Mashariki ya Kati cha Taasisi ya Utafiti ya Marekani limetangaza habari ya kufanyika kongamano la kuipinga Israel mjini Washington.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 03, 2018 12:46 UTC
  • Kongamano la kuwapinga Wazayuni wa Israel lafanyika nchini Marekani

Jarida la Washington Report kwa kushirikiana na kitengo cha Mashariki ya Kati cha Taasisi ya Utafiti ya Marekani limetangaza habari ya kufanyika kongamano la kuipinga Israel mjini Washington.

Kongambano hilo la siku moja la lililo dhidi ya Wazayuni limefanyika chini ya kaulimbiu ya "Ushawishi wa lobi zinazoiunga mkono Israel na taathira zake katika siasa za mambo ya nje za Marekani," limefanyika leo mjini Washington.

Wazungumzaji katika kongamano hilo ambao wengi wao ni watu wa vyuo vikuu na waandishi wa magazeti wa nchi za Magharibi, wamezungumzia taathira za kiistratijia, siasa na hila zinazotumiwa na lobi za Kizayuni kuathiri maamuzi ya Baraza la Congress na idara za serikali ya Marekani.

Maandamano ya kupinga Israel nchini Marekani

 

Waitishaji wa kongamano hilo wanasema kuwa, kadiri siku zinavyopita, ndivyo Wamarekani wanavyozidi kuamka na kuzielewa hila hizo za lobi za Kizayuni na hivi sasa karibu asilimia 85 ya wananchi wa Marekani wanapinga kiwango cha misaada ya Marekani kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Itakumbukwa kuwa kiwango cha misaada isiyo ya kijeshi na kifedha ya Marekani kwa Wazayuni kimeshafikia thamani ya dola bilioni 250 tangu ulipoanzishwa utawala pandikizi wa Israel katika ardhi za Wapalestina mwaka 1948. 

Naam, misaada hiyo haijumulishi ya kijeshi na kifedha ya Marekani kwa utawala wa Kizayuni wa Israel unaotenda jinai za kupindukia dhidi ya Wapalestina.