Kushadidi vita vya kidiplomasia vya nchi za Magharibi dhidi ya Russia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i42262-kushadidi_vita_vya_kidiplomasia_vya_nchi_za_magharibi_dhidi_ya_russia
Maria Zakharova Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesema kuwa, Marekani na Uingereza ni vinara wa uchochezi kuhusu kadhia ya Salisbury, inayomhusu Sergei Skripal jasusi wa zamani wa pande mbili aliyepewa sumu. Amesema Moscow itachukua hatua za kukabiliana na kila nchi ambayo itafuata mkumbo wa Marekani na Russia katika kuwafukuza wanadiplomasia wa Russia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 27, 2018 03:10 UTC
  • Kushadidi vita vya kidiplomasia vya nchi za Magharibi dhidi ya Russia

Maria Zakharova Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesema kuwa, Marekani na Uingereza ni vinara wa uchochezi kuhusu kadhia ya Salisbury, inayomhusu Sergei Skripal jasusi wa zamani wa pande mbili aliyepewa sumu. Amesema Moscow itachukua hatua za kukabiliana na kila nchi ambayo itafuata mkumbo wa Marekani na Russia katika kuwafukuza wanadiplomasia wa Russia.

Siku ya Jumatatu, Marekani ilitangaza kuwa itawatimua wanadiplomasia 60 wa Russia wanaoishi Marekani wakiwemo wanadiplomasia 12 wa Russia walioko katika ubalozi wa kudumu wa nchi hiyo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Hali kadhalika nchi 17 wanachama wa Umoja wa Ulaya pamoja na Australia, Canada na Ukraine nazo pia zimetangaza kuwatimua wanadilomasia wa Russia kwa lengo la kufungamana na Uingereza katika kadhia hiyo ya Skripa ambaye ni raia wa Russia aliyekuwa akiishi uhamishoni Uingereza.

Kwa ujumla wanadiplomasia zaidi ya 100 wa Russia wametimuliwa kutoka nchi hizo. Uingereza siku chache zilizopita nayo pia ilitangaza kuwatimua wanadiplomasia 23 wa Russia. Katika kujibu uhasama huo, Russia nayo ilitangaza kuwatimua wanadiplomasia 23 wa Uingereza mbali na kufunga kituo cha utamaduni cha nchi hiyo maarufu kama British Council mjini Moscow.

Sergei Skripal na binti yake

Kwa mtazamo wa wakuu wa Russia, uchochezi huo wa nchi za Magharibi ambao umeratibiwa kwa njia maalumu unefanyika la lengo la kuishinikiza Russia na kuitenga nchi hiyo katika uga wa kimataifa.

Kama alivyosema Maria Zakharova, nyuma ya pazia ya mashinikizo hayo ni Marekani na Uingereza. Aidha amesema  anaamini kuwa, Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi, NATO ndiye mchochezi mkuu katika Umoja wa Ulaya kwa lengo la kuiharibia jina Russia.  

Wataalamu wa masuala ya kimataifa wanaamini kuwa faili la jasusi Sergei Skripal ni kisingizo ambacho kimetumiwa kwa lengo la kupanua zaidi wigo wa NATO na kuongoeza uchochezi wa kijeshi dhidi ya Russia. Amesema madola ya Magharibi yameanzisha vita vya pande kadhaa dhidi ya Russia. Vita hivyo ni vya kisiasa, vita vya silaha na vita vya mitandao ya intaneti.

Uingereza hadi sasa imekataa kutoa ushahidi wowote kuhusu madai ya kuhusika Russia katika kumpa sumu Skripal na binti yake. Wakuu wa Russia wametaka Uigereza itoe ushahidi lakini jitihada zao zimegonga mwamba.

Kwa mujibu wa Leonid Rink, mtaalamu wa masuala ya kemikali, Russia haikuwa na manufaa yoyote katika kumpa sumu Skripal. Aidha anasema kwa kuzingatia kuwa Russia hivi akribuni imekuwa na uchaguzi wa rais na itandaa kombe la dunia mwaka huu, wakuu wa Moscow hawakuwa na maslahi ya kuchukua hatua kama hivyo katika kipindi hiki muhimu sana.

Maria Zakharova, msemaji wa waizara ya mambo ya nje ya Russia

Jambo ambalo hatupaswi kulisahau ni hili kuwa, kwa kuzingatia hivi sasa Uingereza inakosolewa vikali kutokana na uamuzi wake wa kujiondoa Umoja wa Ulaya katika hatua ambayo ni maarufu kama Brexit, wakuu wa London sasa wanakuza kupita kiasi kadhia ya jasusi Skripal kupewa sumu ya kemikali. Kufuatia kuibuka kadhia hiyo, hivi sasa Uingereza imeweza kuzivutia tena nchi za Ulaya upande wake na pia wakati huo huo kuimarisha uhusiano wake na Marekani uliokuwa umevurugika kufuatia maandamano makubwa yaliyofanyika London kupinga safari ya Rais Donald Trump wa Marekani nchini humo. Upinzani huo ulipelekea Trump avunje safari yake  Uingereza na hivyo kuvuruga uhusiano wa pande mbili. Hivi sasa nchi za Magharibi, kama zinavyokiri zenyewe zinakiri, zimepata kisingizio kizuri cha kueneza propagnada za kisiasa, kidiplopmasia na kihabari dhidi ya Russia na kwa msingi huo msuguano wa pande mbili hizo unatazamiwa kuwa mbaya zaidi katika siku za usoni.