Wanaharakati wa haki za binadamu Ulaya wawaunga mkono mashahidi wa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/world-i45090-wanaharakati_wa_haki_za_binadamu_ulaya_wawaunga_mkono_mashahidi_wa_palestina
Wanaharakati wa haki za binadamu mjini Brussels Ubelgiji wameweka pea 4500 za viatu mbele ya jengo la Baraza la Umoja wa Ulaya ikiwa ni katika kuwaunga mkono wananchi wa Palestina wanaouliwa shahidi kila leo na wanajeshi katili wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 28, 2018 10:29 UTC
  • Wanaharakati wa haki za binadamu Ulaya wawaunga mkono mashahidi wa Palestina

Wanaharakati wa haki za binadamu mjini Brussels Ubelgiji wameweka pea 4500 za viatu mbele ya jengo la Baraza la Umoja wa Ulaya ikiwa ni katika kuwaunga mkono wananchi wa Palestina wanaouliwa shahidi kila leo na wanajeshi katili wa Israel.

Wanaharakati hao wamesema kuwa, wameweka pea hizo 4500 za viatu mbele ya jengo la Makao Makuu ya Baraza la Umoja wa Ulaya mjini Brussels Ubelgiji kama ishara kuwa wako pamoja na mashahidi wa Palestina. 

Christoph Scott, mmoja wa wanaharakati wa haki za binadamu amesema kuwa, kila pea moja ya viatu hivyo inawakilisha roho ya Mpalestina mmoja ambao wameuliwa kidhumla na Israel katika miongo iliyopita. Amesema, zaidi ya pea elfu moja za viatu hivyo ni vya watoto wadogo.

Sehemu ya  pea 4500 za viatu zilizowekwa na wanaharakati wa Ulaya mbele ya jengo la Umoja wa Ulaya mjini Brussels Ubelgiji kutangaza uungaji mkono wao kwa raia wa Palestina wanaouliwa shahidi kila leo na Israel

 

Mwanaharakati huo wa haki za binadamu wa barani Ulaya amesema, lazima utawala wa Kizayuni wa Israel uwekewe vikwazo.

Tangu mwaka 2006 Ukanda wa Ghaza umezingirwa kila upande na Israel kutokea ardhini, angani na baharini baada ya wananchi wa ukanda huo kutumia haki yao ya kidemokrasia ya kuichagua Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS kuwaongoza. 

Tangu tarehe 30 Machi siku iliyosadifiana na maadhimisho ya Siku ya Ardhi, Wapalestina wa Ghaza wamekuwa wakifanya maandamano ya kupigania haki ya wakimbizi wa Palestina ya kurejea katika ardhi zao za jadi zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni. Hadi hivi sasa zaidi ya Wapalestina 120 wameshauliwa shahidi na wanajeshi dhalimu wa Israel na maelfu ya wengine wameshajeruhiwa.