Italia yataka kutatuliwa haraka mgogoro wa wahajiri haramu waliokwama melini
https://parstoday.ir/sw/news/world-i47611-italia_yataka_kutatuliwa_haraka_mgogoro_wa_wahajiri_haramu_waliokwama_melini
Serikali ya Italia imetaka kutatuliwa suala la mamia ya wahajiri haramu waliokwama melini katika kisiwa cha Sicilian mjini Catania na kusema kuwa, viongozi wa nchi za Ulaya wanapaswa kuutatua haraka mgogoro huo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 22, 2018 14:25 UTC
  • Italia yataka kutatuliwa haraka mgogoro wa wahajiri haramu waliokwama melini

Serikali ya Italia imetaka kutatuliwa suala la mamia ya wahajiri haramu waliokwama melini katika kisiwa cha Sicilian mjini Catania na kusema kuwa, viongozi wa nchi za Ulaya wanapaswa kuutatua haraka mgogoro huo.

Leo serikali ya Italia imeelezea matumaini yake ya kujulikana haraka hatima ya wahajiri 177 haramu ambao tangu wiki moja nyuma wamekwama ndani ya meli katika fukwe za nchi hiyo. Matamshi hayo yamekuja huku baadhi ya duru zikiishutumu Italia kuwa imewateka nyara wahajiri hao.

Jumatano iliyopita ya Tarehe 15 mwezi huu, wahajiri hao 177 walipelekwa katika fukwe za Italia baada ya kuokolewa baharini. Hata hivyo serikali ya nchi hiyo imekataa kuwapokea na kuwakaribisha wahajiri hao katika ardhi ya Italia na imezitaka nchi nyingine za Ulaya kama Ujerumani na Ufaransa ziwape hifadhi wahajiri hao.

Baadhi ya wakimbizi 177 waliokwama melini huko Cecilia, Italia

 

Ijapokuwa kumeshafanyika mazungumzo mengi kuhusu wakimbizi wanaoingia Italia, lakini nchi nyingine za Ulaya hadi sasa hazijachukua hatua yoyote ya maana ya kupokea wahajiri hao.

Hivi sasa Italia imeamua kuweka sheria kali za kupambana na vimbi kubwa la wahajiri wanaoingia nchini humo kinyume cha sheria. Matumaini ya serikali ya Italia kupitia sheria hizo kali ni kuhakikisha inafuta kabisa uwezekano wa wahajiri haramu kuingia nchini humo.