Korea Kaskazini: Tutaendelea na mpango wa kuangamiza silaha za nyuklia
(last modified Fri, 07 Sep 2018 04:47:33 GMT )
Sep 07, 2018 04:47 UTC
  • Korea Kaskazini: Tutaendelea na mpango wa kuangamiza silaha za nyuklia

Kwa mara nyingine Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini amesisitiza kuwa nchi yake itaendelea kufungamana na majukumu yake ya kuangamiza silaha zake za nyuklia na kuimarisha usalama katika Rasi ya Korea.

Jong-un aliyasema hayo alipokutana na Chung Eui-yong, mjumbe maalumu wa Rais wa Korea Kusini mjini Pyongyang na kuongeza kuwa, kuondolewa hatari ya vita katika Rasi ya Korea, bila kuwepo silaha na vitisho vya nyuklia, ni katika maudhui ambazo Korea Kaskazini imeendelea kufungamana nazo. Kim Jong-un amesema kuwa, kupatikana Rasi ya Korea isiyo na silaha za nyuklia, ni sababu ya kustawisha uhusiano wa Korea mbili. Kiongozi wa Korea Kaskazini amefafanua kwamba, anataka kuharakishwa utekelezwaji wa masuala yanayohusiana na ustawishaji wa uhusiano wa nchi mbili na kulindwa usalama na uthabiti wa eneo la Korea.

Chung Eui-yong, mjumbe maalumu wa rais wa Korea Kusini alipokutana na Kim Jong-un

Chung Eui-yong, mjumbe maalumu wa rais wa Korea Kusini ambaye pia ni Mkuu wa Ofisi ya Usalama wa Taifa katika ikulu ya Rais Moon Jae-in alifanya safari mjini Pyongyang siku ya Jumatano kwa ajili ya kuwasilisha barua kutoka kwa Rais Jae-in. Akizungumzia ujumbe uliokuwa ndani ya barua, Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini amesema kuwa, barua hiyo imebainisha mwanga katika mustakbali wa uhusiano wa Korea mbili. Kikao cha tatu cha viongozi wa nchi mbili kimepangwa kufanyika kati ya tarehe 18 na 20 ya mwezi huu mjini Pyongyang.

Tags