Uchaguzi Ukraine : Mchekeshaji Zelensky ashinda kiti cha urais
https://parstoday.ir/sw/news/world-i53007-uchaguzi_ukraine_mchekeshaji_zelensky_ashinda_kiti_cha_urais
Msanii mchekeshaji wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa rais, kutokana na kura zilizopigwa.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Apr 22, 2019 00:06 UTC
  • Uchaguzi Ukraine : Mchekeshaji Zelensky ashinda kiti cha urais

Msanii mchekeshaji wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa rais, kutokana na kura zilizopigwa.

Matokeo ya uchaguzi huo yanaonyesha kuwa, Volodymyr Zelensky amepata zaidi ya asilimia 70 yya kura na hivyo kupata nafasi ya kuongoza nchi hiyo.

Volodymyr Zelensky mwenye umri wa miaka 41, ammebwaga na kumuondoa madarakani Rais Petro Poroshenko ambaye amekubali kushindwa.

Matokeo ya sasa yanaonekana kuwa ni pigo kubwa kwa bwana Poroshenko na kukataliwa kuanzishwa kwa Ukraine mpya.

"Sitawaangusha ," Bwana Zelensky aliwaambia waliomuunga mkono wakati wa sherehe za kujipongeza.

Zoezi la upigaji kura nchini Ukraine

Aliongeza kusema "Sijawa rais bado lakini kama raia wa Ukraine, ninaweza kuwaambia nchi zote za Kisovieti kuwa watuangalie sisi, Kila kitu kinawezekana".

Zelensky anajulikana kwa umahiri wa ucheshi wake kama muigizaji nyota wa mfululizo wa filamu ya satirical katika television ambapo anaigiza kama rais wa Ukraine.

Rais ana mamlaka makubwa katika upande wa usalama, jeshi na sera za kigeni katika nchi hiyo.

Akizungumza baada ya kutangazwa matokeo hayo, Rais wa sasa wa Ukraine anayeondoka madarakani amewaambia waandishi wa habari kwamba, nimekubali matokeo na nitaondoka madarakani lakini sitaacha siasa.

Duru ya pili ya uchaguzi wa Rais nchini Ukraine ilifanyika jana Jumapili baada ya duru ya kwanza kushindwa kutoa mshindi.