China na Korea Kaskazini zakosoa siasa za kimabavu za Marekani
(last modified Fri, 21 Jun 2019 07:27:57 GMT )
Jun 21, 2019 07:27 UTC
  • China na Korea Kaskazini zakosoa siasa za kimabavu za Marekani

Akizungumza na Rais Xi Jinping wa China, Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini amekosoa vikali siasa za uhasama za Marekani.

Kiongozi wa Korea Kaskazini ameyasema hayo mjini Pyongyang katika kikao na rais wa China ambapo amesema kuwa nchi yake imechukua hatua za lazima kwa ajili ya kuzuia kuibuka mgogoro na Marekani, lakini bado haijapata jibu kutoka kwa Washington. Kadhalika amepongeza nafasi chanya ya China katika utatuzi wa masuala ya Rasi ya Korea na kuongeza kwamba Pyongyang inataka kuendelezwa ushirikiano wa pande mbili na Beijing.

Rais Donald Trump wa Marekani, chanzo cha migogoro duniani

Kwa upande wake Rais Xi Jinping wa China amesema kuwa, Beijing inaiunga mkono Korea Kaskazini katika njia ya utatuzi wa masuala ya nyuklia katika eneo hilo. Amepongeza juhudi za Pyongyang za kuinua kiwango cha usalama na uthabiti na hatua yake ya kutokomeza silaha za nyuklia katika na eneo la Korea na kusisitizia umuhimu wa kupanuliwa ushirikiano wa nchi hizo. Safari ya Rais Xi Jinping nchini Korea Kaskazini ni safari yake ya kwanza tangu alipoingia madarakani mwaka 2013, kama ambavyo ni safari ya kwanza ya kiongozi wa ngazi ya juu wa China nchini humo katika kipindi cha miaka 14 iliyopita. 

Tags