Kushner akiri: Mkutano wa kuzindua "Muamala wa Karne" Bahrain umefeli
https://parstoday.ir/sw/news/world-i54630-kushner_akiri_mkutano_wa_kuzindua_muamala_wa_karne_bahrain_umefeli
Jared Kushner, mkwe wa Rais Donald Trump wa Marekani amekiri kwamba, Waplestina wameufanya mkutano wa kiuchumi wa Bahrain, uliokuwa umeitishwa kuzindua mpango wa Mualama wa Karne dhidi ya taifa la Palestina, ushindwe na kufeli.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 08, 2019 10:36 UTC
  • Kushner akiri: Mkutano wa kuzindua

Jared Kushner, mkwe wa Rais Donald Trump wa Marekani amekiri kwamba, Waplestina wameufanya mkutano wa kiuchumi wa Bahrain, uliokuwa umeitishwa kuzindua mpango wa Mualama wa Karne dhidi ya taifa la Palestina, ushindwe na kufeli.

Gazeti la Kizayuni la Haaretz limemnukuu Jared Kushner akisema viongozi wa makundi mbalimbali ya Palestina wameufanya mkutano wa Manama ushindwe na kugonga ukuta kwa kuwawekea mashinikizo wafanyabiashara na washiriki katika mkutano huo.  

Mkutano wa kiuchumi wa Manama huko Bahrain ambao ulikuwa hatua ya kwanza ya kutekeleza mpango wa Kimarekani wa eti "Muamala wa Karne" ulifanyika tarehe 25 na 26 za mwezi uliopita wa Juni licha ya upinzani mkubwa wa kikanda na kimataifa. 

Nchi nyingi za Waislamu na zisizo za Waislamu na makundi na harakati zote za Palestina zilisusia mkutano huo. 

Mpango wa Muamala wa Karne ni njama mpya iliyobuniwa na serikali ya Marekani kwa lengo la kuzima na kutokomeza kabisa haki za taifa la Palestina. Mpango huo umebuniwa na Marekani kwa kushirikiana na vibaraka wake kama Saudi Arabia, Bahrain na Imarati. 

Kushner akiwa pamoja na mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia, Bin Salman

Kwa mujibu wa mpango huo, Quds tukufu na kibla cha kwanza cha Waislamu kitakabidhiwa kwa utawala wa Kizayuni wa Israel, wakimbizi wa Palestina hawataruhusiwa kurejea katika nchi yao iliyoghusubiwa na Palestina itakuwa na ardhi ndogo iliyobakia katika Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza.