Maduro afichua mpango wa Marekani na Colombia wa kutaka kumuuwa
(last modified Mon, 23 Sep 2019 02:47:21 GMT )
Sep 23, 2019 02:47 UTC
  • Nicolas Maduro
    Nicolas Maduro

Rais wa Venezuela amefichua mpango wa kutaka kumuuwa unaofanywa kwa siri na rais wa zamani wa Colombia kwa kushirikiana na Marekani.

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela amesema kuwa hadi sasa njama kadhaa zimezimwa na kusambaratishwa za kutaka kumuuwa likiwemo shambulio la droni la mwezi Agost mwaka jana katika mji mkuu Caracas.  Rais wa Venezuela ameongeza kuwa, inasikitisha kuona kuwa, pande hizo zinatumia mbinu za siri ili kumuondoa madarakani kwa kutekeleza mauaji ya kisiasa. Kabla ya tukio hili pia, Rais Maduro aliwahi kusema kuwa, Colombia imepanga njama kumi za kumuuwa. 

Rais wa Venezuela amesema kuwa, Marekani na rais wa zamani wa Colombia Alvaro Uribe walihusika katia njama zote hizo. Marekani ilijaribu kufanya mapinduzi nchini Venezuela katika miezi kadhaa ya karibuni na inaendelea kuwaunga mkono wapinzani wa serikali halali ya Caracas. 

Alvaro Uribe, rais wa zamani wa Colombia
 

Marekani pia ina lengo la kuiwekea Venezuela mzingiro wa baharini ili kuiangusha serikali halali iliyoko madarakani sambamba na kuiwekea nchi hiyo vikwazo vikali vya kiuchumi.  

Tags