Nov 13, 2019 02:33 UTC
  • Putin na Merkel wataka wakimbizi wa Syria warejeshwe katika makazi yao

Rais Vladimir Putin wa Russia na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wamesisitiza udharura wa kurejeshwa wakimbizi wa Syria katika makazo na maeneo yao.

Katika mazungumzo yao ya simu, viongozi hao wawili wamesema kuwa, pande mbili zinataka wakimbizi wa Syria warejeshwe katika maeneo yao na kutilia mkazo umuhimu wa kutatuliwa matatizo ya kibinadamu huko Syria. 

Taarifa iliyotolea na Ikulu ya Rais wa Russia, Kremlin imesema kuwa, Berlin na Moscow pia zinataka kusitishwa vita mara moja na bila ya masharti nchini Libya.

Wakimbizi wa Syria

Kabla ya mazungumzo hayo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya, Fathi Bashagha alikuwa ameituhumu Russia kuwa inafanya njama za kurejesha madarakani mabaki ya utawala wa dikteta wa zamani wa nchi hiyo, Muammar Gaddafi.   

Tarehe 4 Aprili mwaka huu wapiganaji wa lile linalojiita jeshi la taifa la Libya linaloongozwa na Khalifa Haftar anayeungwa mkono na kusaidiwa na Saudi Arabia, Imarati, Misri na baadhi ya nchi za Magharibi, walianzisha mashambulizi makali dhidi ya mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli. Mashambulizi hayo yamesababisha mauaji ya raia wasiopungua 1090 na kuzidisha mgogoro wa ndani wa Libya. 

Tags