Trump alishauriana na Michel Temer kuivamia kijeshi Venezuela
(last modified Thu, 28 Nov 2019 10:25:11 GMT )
Nov 28, 2019 10:25 UTC
  • Trump alishauriana na Michel Temer kuivamia kijeshi Venezuela

Rais wa zamani wa Brazil, Michel Temer, amesema kuwa, Rais wa Marekani alimuuliza kuhusu namna ya kuishambulia Venezuela.

Amesema, wakati alipokuwa Rais wa Brazil,  Rais Donald Trump wa Marekanii aliwaalika katika chakula cha usiku yeye pamoja na Juan Manuel Santos Rais wa wakati huo wa Colombia na Juan Carlos Varela Rais wa zamani wa Panama ili kuzungumzia namna wanavyoweza kuivamia kijeshi Venezuela. 

Temer amesema kama ninavyomnukuu: "Mimi na Santos tulimweleza Trump kwamba ni bora uchukuliwe msimamo wa kidiplomasia na tuepuke hatua ya kijeshi." Mazungumzo hayo yalifanyika pambizoni mwa kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York,  Marekani mwaka 2017. 

Temer ameongeza kuwa, Venezuela ilikuwa moja ya matatizo makuu ya serikali yake kimataifa. Michel Temer aliingia madarakani huko Brazil mwaka 2016 baada ya kuuzuliwa Dilma Rousseff rais wa wakati huo wa nchi hiyo. 

Marekani na waitifaki wake katika miaka ya karibuni wameiweka Venezuela chini ya mashinikizo makali ya kiuchumi na kisiasa lengo lao likiwa ni kuipindua serikali halali ya Rais Nicolaus Maduro. 

Rais Nicolaus Maduro wa Venezuela 
 

 

Tags