Venezuela: Vikwazo vya Marekani ni jinai dhidi ya ubinadamu
(last modified Sun, 08 Mar 2020 08:05:09 GMT )
Mar 08, 2020 08:05 UTC
  • Venezuela: Vikwazo vya Marekani ni jinai dhidi ya ubinadamu

Makamu wa Rais wa Venezuela amelaani vikwazo vya upande mmoja vya serikali ya Marekani dhidi ya nchi yake na kuvitaja kuwa dhidi ya ubinadamu.

Delcy Rodriguez ameashiria hatua ya Venezuela ya kuishtaki Marekani katika mahakama ya ICC na kueleza kuwa vikwazo vya mabavu na upande mmoja vya serikali ya Marekani dhidi ya nchi yake vimegeuzwa na kuwa silaha ya kuwaangamiza wananchi.  

Makamu wa Rais wa Venezuela amezitathimini pia siasa za nje za Marekani na kuzitaja kuwa ni kinyume cha seria na zinazokinzana na misingi ya haki za kimataifa. Rais Nicolas Maduro wa Venezuela tarehe 13 mwezi Februari mwaka huu alitangaza kuwa nchi hiyo imewasilisha kwa mahakama ya ICC faili la hatua na vikwazo vya upande mmoja vya Washington dhidi ya Caracas. Rais Maduro alizitaja hatua hizo na vikwazo vya upande mmoja vya Marekani dhidi ya nchi yake kuwa dhidi ya ubinadamu na kusisitiza kuwa wananchi wa Venezuela wana haki ya kuishi kwa amani na kujitawala nchini kwao. 

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela  

Venezuela imekumbwa na vikwazo vikali vya kiuchumi vya Marekani kuwahi kushuhudiwa katika miongo kadhaa iliyopita tangu Donald Trump aingie madarakani huko White House. 

Tags