Russia yasajili dawa nyingine ya kutibu corona
Wizara ya Afya ya Russia imetangaza kwamba imesajili dawa nyingine iliyopewa jina la Levilimab kwa ajili ya kutibu wagonjwa wahututi wa corona.
Taarifa ya Wizara ya Afya ya Russia imetangazwa kuwa, dawa hiyo itasambazwa kwa kutumia jina la kibiashara la Ilsira na kwamba itatumika kwa ajili ya kutibu wagonjwa mahututi wa virusi vya corona na ina taathira kubwa katika kutibu sehemu zilizoshambuliwa na virusi hivyo hususan mapafu.
Siku chache zilizopita Wizara ya Afya ya Russia ilikuwa imetangaza kuwa imesajili dawa na kutibu wagonjwa wa corona ya Avifavir.
Afrisa mmoja wa Russia amesema hadi sasa nchi hiyo imetengeneza mifuko elfu 18 ya dawa ya Avifavir na kwamba ina uwezo wa kuzalisha mifuko 720 ya dawa hiyo.
Zaidi ya Warusi 467,673 wamepatwa na virusi vya corona na 5,859 miongoni mwao wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo.