Watu karibu milioni moja wameambukizwa corona nchini Brazil
https://parstoday.ir/sw/news/world-i61680-watu_karibu_milioni_moja_wameambukizwa_corona_nchini_brazil
Idadi ya watu waliopatwa na virusi vya corona nchini Brazil imefika milioni moja.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 18, 2020 11:08 UTC
  • Makaburi ya wahanga wa corona, Brazil
    Makaburi ya wahanga wa corona, Brazil

Idadi ya watu waliopatwa na virusi vya corona nchini Brazil imefika milioni moja.

Wizara ya Afya ya Brazil, kwa kuzingatia mwenendo wa kasi ya maambukizi ya virusi vya corona nchini humo imetangaza kuwa, katika muda wa masaa 24 yaliyopita imesajili kesi mpya 32,188 za maambukizi ya corona na hivyo kuifanya idadi jumla ya maambukizi ya corona nchini humo kufikia 960,309. 

Brazil inashika nafasi ya pili kwa kuwa na idadi kubwa ya watu walioaga dunia kwa corona baada ya Marekani 

Wizara ya Afya ya Brazil imeongeza kuwa idadi ya watu walioaga dunia kwa corona nchini humo imeongezeka na kuwa 46,665 baada ya kusajiliwa watu 1,269 waliopoteza maisha kwa corona katika masaa 24 yaliyopita. 

Brazil inashika nafasi ya pili baada ya Marekani kwa kuwa na idadi kubwa ya watu walioambukizwa virusi vya corona na pia wale walioaga dunia kwa maradhi ya Covid-19.  

Ripoti zinaeleza kuwa, hospitali nchini Brazil zinakabiliwa na matatizo mengi ya uhaba wa vifaa tiba na vile vya kuwahudumia wagonjwa wapya wanaofika hospitalini.