Maduro: Guaido naye amembwaga Trump
(last modified Mon, 09 Nov 2020 12:01:55 GMT )
Nov 09, 2020 12:01 UTC
  •  Nicolas Maduro
    Nicolas Maduro

Rais wa Venezuela amesema kuwa katika kipindi cha miaka miwili ilimpatia serikali ya Donald Trump mwanasiasa aliyejitangaza kuwa rais wa Venezuela kiasi cha dola milioni 800 lakini hatimaye mwanasiasa huyo, Juan Guaido, pia amemsalitia Trump.

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela amesema kuwa serikali ya Rais Donald Trump ndiyo iliyomtengeneza Juan Guaido, kibaraka wa Washington aliyejitangaza kuwa rais wa Venezuela, na katika muda wa miaka miwili iliyopita imempatia dola milioni 800; hata hivyo Guaido hatimaye amemsaliti Trump baada ya ushindi wa Joe Biden katika uchaguzi wa rais wa Marekani. 

Juan Guaido, aliyejitangaza rais wa Venezuela 

Serikali ya Trump ilifanya juhudi kubwa za kumuondoa madarakani Rais Nicolas Maduro ikiwa ni pamoja na kutumia wenzo wa vikwazo na mashinikizo na hata jaribio la mapinduzi nchini Venezuela lakini njama zote hizo zimeambulia patupu.   

Rais Maduro wa Venezuela pia aliudhihaki mchakato wa uchaguzi wa rais nchini Marekani. hata hivyo amewapongeza rais mteule, Joe Biden na makamuu wake Kamala Harris kwa kuibuka na ushindi katika uchaguzi huo na kusisitiza kuwa, Venezuela ipo tayari kufanya mazungumzo na wananchi na serikali ya Marekani. 

Tags