Kuendelea vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu nchini Sweden
https://parstoday.ir/sw/news/world-i64680-kuendelea_vitendo_vya_chuki_dhidi_ya_uislamu_nchini_sweden
Mwendesha Mashtaka wa Sweden amesema kuwa kuchomwa moto kitabu kitakatifu cha Qur'ani si hatia na hivyo kusimamisha uchunguzi uliokuwa ukiendelea juu ya kuvunjiwa heshima kitabu hicho kitakatifu cha Waislamu.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Nov 17, 2020 12:24 UTC
  • Kuendelea vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu nchini Sweden

Mwendesha Mashtaka wa Sweden amesema kuwa kuchomwa moto kitabu kitakatifu cha Qur'ani si hatia na hivyo kusimamisha uchunguzi uliokuwa ukiendelea juu ya kuvunjiwa heshima kitabu hicho kitakatifu cha Waislamu.

Kwa mujibu wa shirika la Reuters, mwendesha mashtaka huyo amedai kwamba kuteketezwa kibu hicho cha mbinguni hakuendi kinyume cha sheria wala kuchukuliwa kuwa kosa na hivyo kusimamisha uchunguzi ambao umekuwa ukiendelea katika uwanja huo tokea mwezi Agosti uliopita.

Akizungumza leo Jumanne na televisheni ya taifa ya Sweden, Sofia Siren mwendesha mshtaka wa nchi hiyo amedai kwamba hakuna uwezekano wowote wa kuthibitisha hatia kuhusu suala hilo kwa madai kuwa nafsi ya kitendo cha kuchomwa moto Qur'ani si jambo linalokwenda kinyume na sheria za nchi hiyo.

Wakati huo huo ameongeza kuwa hata kama kuchomwa moto Qur'ani ni kitendo ambacho kimefanyika dhidi ya jamii moja ya nchi hiyo lakini waliohusika na kitendo hicho hawajulikani waliko.

Waungaji mkono wa chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu

Siku chache zilizopita polisi ya Sweden ilitangaza kuwa msikiti mkuu wa Ijumaa wa nchi hiyo na misikiti mingine minne ilipokea barua za vitisho.

Katika miezi iliyopita Sweden imeshuhidia vitendo kadhaa vya Waislamu kushambuliwa na maeneo yao ya ibada pamoja na matukufu yao kikiwemo kitabu kitakatifu cha Qur'ani kuvunjiwa heshima.

Siku kadhaa zilizopita pia, mtu mmoja mwenye chuki kali dhidi ya Uislamu aliteketeza Qur'ani Tukufu katika mtaa wa wakazi wenye chuki kali dhidi ya Uislamu na Waislamu wa Rinleby katika mji mkuu, Stockholm.

Waislamu nchini humo wamekuwa wakibainisha wasiwasi wao mkubwa kuhusiana na vitendo vya chuki vinavyowalenga pamoja na maeneo yao ya ibada, na kutaka hatua za dharura zichukuliwe na maafisa husika kwa ajili ya kuwalinda.