Jan 18, 2021 08:17 UTC
  • Viongozi wa Ufaransa waifunga misikiti 9 nchini humo

Viongozi wa Ufaransa wameifunga misikiti 9 nchini humo katika kuendelea sera za chuki za serikali ya Paris dhidi ya Uislamu.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ufaransa jana ilitangaza taarifa ya kufungwa misikiti 9 kwa kisingizio cha kupambana na kile ilichokitaja kuwa hatua za Waislamu za kutaka kujitenga. Gérald Darmanin Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa pia  ameandika katika ukurasa wake wa twitter kwamba: Misikiti 9 imefungwa nchini humo kati ya misikiti na maeneo ya kuswalia18 ambayo aliagiza kuwekwa chini ya udhibiti mkali. 

Darmanin tarehe Pili Disemba mwaka jana pia alitangaza habari ya kuchukuliwa hatua kubwa na kali za kuidhibiti misikiti 76 huko Ufaransa. 

Maeneo ya kidini ya kufanyika ibada ya Waislamu huko Ufaransa katika wiki za karibuni  yalifanyiwa uchunguzi mara 34.  

Muswada wa sheria kwa ajili ya kuzingatia sheria mpya ya mfumo wa Jamhuri nchini Ufaransa inayokabiliana na hatua za wanaotaka kujitenga leo itawasilishwa kwa wabunge wa Ufaransa ili kuchunguzwa na Kamati Maalumu ya Bunge.  

Muswada huo utaanza kujadiliwa katika bunge la Ufaransa kuanzia Februari Mosi mwaka huu. Serikali ya Ufaransa katika miezi ya karibuni imetekeleza vizuizi na hatua kali dhidi ya Waislamu nchini humo. Kitendo cha Rais Emmanuel Macron wa nchi hiyo cha kuunga mkono kuchapishwa vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume Mtukufu wa Uislamu (S.A.W) kimepingwa na kulaaniwa vikali katika Ulimwengu wa Kiislamu. 

Maandamano dhidi ya Macron katika ulimwengu wa Kiislamu 

 

Tags