Wingu la umasikini limegubika maisha ya Wamarekani milioni 55
https://parstoday.ir/sw/news/world-i67620-wingu_la_umasikini_limegubika_maisha_ya_wamarekani_milioni_55
Vyombo vya habari nchini Marekani vimetangaza kuwa sudusi moja ya watu wa nchi hiyo hawana uhakika wa kupata chakula.
(last modified 2026-05-06T11:35:21+00:00 )
Mar 07, 2021 10:18 UTC
  • Wingu la umasikini limegubika maisha ya Wamarekani milioni 55

Vyombo vya habari nchini Marekani vimetangaza kuwa sudusi moja ya watu wa nchi hiyo hawana uhakika wa kupata chakula.

Kwa mujibu wa kanali ya televisheni ya MSNBC News, kuna maeneo nchini Marekani ambayo wakazi wake wanapopata mlo mmoja wa chakula huwa hawajui kama je wataweza kupata mlo mwengine unaofuata au la. 

Kanali hiyo ya televisheni imetangaza kuwa, kutokana na bima ya huduma za matibabu ya raia wengi wa Marekani kuwa na uhusiano na suala la ajira, hivi sasa watu milioni 29 nchini humo wameshindwa kuwa na bima hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Wamarekani zaidi ya milioni 40 ambao ni wapangaji hawana uwezo wa kulipa kodi za nyumba wakiwa na hofu na wasiwasi wa kuhamishiwa vyombo vyao katika nyumba walizopanga.

Bernie Sanders

Hivi karibuni, Bernie Sanders, Seneta wa jimbo la Vermont alitoa mkanda wa video ambao ndani yake amekosoa sera mbovu za kiuchumi nchini Marekani na kubainisha kuwa, sera mbovu za kiuchumi nchini humo zimeifanya asilimia moja tu ya jamii ya nchi hiyo kuwa tajiri zaidi na yenye uwezo mkubwa zaidi na kulifanya tabaka la wafanyakazi wa vibarua libaki mikono mitupu.

Kiwango cha umasikini kinaongezeka nchini Marekani wakati kipindi cha utoaji msaada maalum wa kifedha wa serikali kutokana na usambaaji wa virusi vya corona kilimalizika tangu mwisho kwa mwezi Julai mwaka jana, huku mbinyo wa maradhi ya Covid-19 kwa uchumi wa nchi hiyo ukiwa unaendelea.../