Russia: Nato ichague njia ya ama makabiliano au ushirikiano
https://parstoday.ir/sw/news/world-i68292-russia_nato_ichague_njia_ya_ama_makabiliano_au_ushirikiano
Viongozi wa ngazi ya juu wa Russia wamejibu matamshi ya Katibu Mkuu wa Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) kuhusu eti siasa za hujuma za Moscow na kusema Nato yenyewe ndio kitovi kikuu cha vitisho duniani. Wameongeza kuwa Brussels itatue matatizo yanayozikabili nchi wanachama wa muungano wa NATO na iweke wazi msimamo wake kuhusu Moscow.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Mar 25, 2021 11:27 UTC
  • Maria Zakharova
    Maria Zakharova

Viongozi wa ngazi ya juu wa Russia wamejibu matamshi ya Katibu Mkuu wa Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) kuhusu eti siasa za hujuma za Moscow na kusema Nato yenyewe ndio kitovi kikuu cha vitisho duniani. Wameongeza kuwa Brussels itatue matatizo yanayozikabili nchi wanachama wa muungano wa NATO na iweke wazi msimamo wake kuhusu Moscow.

Msemaji Rasmi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia Maria Zakharova amemnasihi Jens Stoltenberg, Katibu Mkuu wa NATO kwamba, badala ya kutoa madai yasiyo na msingi kuhusu Russia atatua matatizo yanayoukabili muungano huo wa kijeshi wa nchi za Magharibi.

Jens Stoltenberg, Katibu Mkuu wa Nato 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amebainisha hayo akijibu matamshi ya Katibu Mkuu wa NATO aliyedai kuwa Moscow inatekeleza siasa za uchokozi. Maria Zakharova amesema kuwa viongozi wa Brussels ni vyema kwanza wayapatia ufumbuzi matatizo ya nchi wanachama wa NATO na kwamba matatizo hayo yanahitaji hatua za haraka. 

Zakharova ameashiria matatizo yaliyopo kuhusiana na chanjo, janga la corona, na ukiukwaji wa wazi wa haki za binadamu katika nchi wanachama wa muungano wa NATO na kueleza kuwa, ni vyema masuala hayo yakapatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

Itakumbukwa kuwa, Katibu Mkuu wa NATO alidai katika kikao na waandishi wa habari huko Brussels kwamba, Russia ni sababu ya ukosefu wa amani unaoshuhudiwa katika nchi jirani na kwamba nchi hiyo inaendelea kuimarisha uwezo wake wa kijeshi na siasa za kichokozi huku ikiwakandamiza wapinzani wa kisiasa wa ndani.