Borell asisitiza ushirikiano wa masharti kati ya Brussels na Taliban
(last modified Wed, 15 Dec 2021 07:23:07 GMT )
Dec 15, 2021 07:23 UTC
  • Josep Borrell
    Josep Borrell

Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema kuwa udharura wa kuwepo ushirikiana na kundi la Taliban lakini ushirikiano huo unapaswa kufanyika kwa masharti.

Josep Borrell ambaye alikuwa akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa mwezi Septemba Umoja wa Ulaya uliaianisha masharti matano kwa ajili ya kushirikiana na kundi la Taliban na kwamba kundi hilo linapasa kupiga hatua katika uwanja huo. 

Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema kushirikiana na Taliban ni jambo la dharura na wakati huo huo ameongeza kuwa mtazamo huo hauhalalishi kundi hilo.

Tarehe 3 Septemba mwaka huu Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya waliainisha mambo matano ambayo yatakuwa msingi wa ushirikiano wa Umoja wa Ulaya na Taliban. 

Kuundwa serikali shirikishi ya kitaifa, kuruhusu misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Ulaya na kuheshimu haki za binadamu hususan haki za wanawake, utawala wa katiba na uhuru wa vyombo vya habari ni kati ya misingi hiyo mikuu iliyoainishwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa EU.

Borrell amesisitiza kuwa Umoja wa Ulaya utapanua ushirikiano wake na waitifaki wake Asia ya Kati na kwamba Afghanistan pia ina umuhimu katika uwanja huo.   

Umoja wa Ulaya umeainisha masharti hayo kwa ajili ya kushirikiana na kundi la Taliban linaloongoza huko Afghanistan katika hali ambayo nchi hiyo sasa inakabiliwa na mgogoro wa kibinadamu.

Maafisa wa kundi la Taliban linaloongoza Afghanistan 

 

Tags