Russia: Shambulio dhidi ya hospitali ya watoto ni "habari feki"
https://parstoday.ir/sw/news/world-i81230-russia_shambulio_dhidi_ya_hospitali_ya_watoto_ni_habari_feki
Russia imekanusha habari kuwa imeshambulia hospitali ya watoto katika mji wa Mariupol nchini Ukraine na kutangaza kuwa, jengo linalodaiwa kushambuliwa lilikuwa liimeshatekwa na askari wake kabla ya shambulio hilo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 10, 2022 08:47 UTC
  • Russia: Shambulio dhidi ya hospitali ya watoto ni

Russia imekanusha habari kuwa imeshambulia hospitali ya watoto katika mji wa Mariupol nchini Ukraine na kutangaza kuwa, jengo linalodaiwa kushambuliwa lilikuwa liimeshatekwa na askari wake kabla ya shambulio hilo.

Dmitry Polyanskiy, naibu wa kwanza wa balozi na mwakilishi wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema katika ujumbe alioandika kwenye mtandao wa kijamii wa twitter, "Russia ilikuwa imeshatahadharisha katika taarifa iliyotoa siku mbili kabla, kwamba hospitali hiyo imegeuzwa eneo la kijeshi na Waukraine wenye misimamo mikali; inasikitisha sana kuona Umoja wa Mataifa unasambaza taarifa hii isiyo na uthibitisho."

Polyasnskiy ameandika twitter hiyo kujibu ujumbe wa twitter pia ulioandikwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Jengo la hospitali ya mjini Mariupol, Ukraine

Kuhusiana na shambulio hilo, Guterres alikuwa ameandika aktika ujumbe wake: "shambulio la siku ya Jumatano dhidi ya hospitali katika mji wa Mariupol, Ukraine, mahali ambapo kuna wadi za wazazi na watoto, linatisha. Ukatili huu usio na maana inapasa usimamishwe."

Baada ya maafisa wa serikali ya Ukraine kutangaza hapo jana kuwa ndege za kivita za Russia zimeshambulia hospitali ya watoto, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenzsky aliituhumu Moscow kuwa imefanya mauaji ya kimbari.../