Baada ya kutelekezwa na Marekani, wakimbizi Waafghani waliokuweko UAE warejea nyumbani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i81410-baada_ya_kutelekezwa_na_marekani_wakimbizi_waafghani_waliokuweko_uae_warejea_nyumbani
Mamia ya wahajiri Waafghani ambao walikuwa wamewekwa kwenye kambi moja nchini Imarati tangu miezi saba nyuma, wakiwa na matumaini ya kusafirishwa kupelekwa Marekani wameamua kurudi nchini kwao Afghanistan kutokana na ukwamishaji ambao Washington imekuwa ikiendelea kuufanya kuhusiana na safari yao.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Mar 15, 2022 13:18 UTC
  • Baada ya kutelekezwa na Marekani, wakimbizi Waafghani waliokuweko UAE warejea nyumbani

Mamia ya wahajiri Waafghani ambao walikuwa wamewekwa kwenye kambi moja nchini Imarati tangu miezi saba nyuma, wakiwa na matumaini ya kusafirishwa kupelekwa Marekani wameamua kurudi nchini kwao Afghanistan kutokana na ukwamishaji ambao Washington imekuwa ikiendelea kuufanya kuhusiana na safari yao.

Waafghani wapatao 300 miongoni mwa maelfu ya wahajiri wa Kiafghani waliihama Afghanistan kupitia operesheni ya jeshi la Marekani iliyopewa jina la "Operesheni ya Uhamishaji" wameamua kurudi nchini mwao kutokana na kutofahamika hatima yao na kuhalifu ahadi serikali ya Washington ya kuwahamisha Imarati na kuwapeleka Marekani.

Wahajiri hao wanasema: raia wa Afghanistan waliopelekwa kwenye kambi za wahajiri mjini Abu Dhabi wamekuwa wakikabiliwa na matatizo mengi; na kwa sababu hiyo wameamua kurudi Afghanistan.

Katika mchakato wa uhamishaji watu Afghanistan, raia wapatao elfu 80, ambao baadhi yao walikuwa wakihudumu katika taasisi za kijeshi za Marekani na nchi zingine za Magharibi, waliihama nchi yao.

Waafghanistan wakiihama nchi yao kwa kutumia ndege ya jeshi la Marekani

 

Ripoti zinaeleza kuwa, kati ya maelfu ya wahajiri Waafghani waliohamishiwa Imarati, Marekani imekubali kuwapokea watu 130 tu, jambo ambalo limewakasirisha sana wahajiri wengine Waafghani.

Kitambo nyuma, Naibu Kaimu Waziri Mkuu wa serikali ya muda ya Taliban Abdul Salam Hanafi alituma salamu kwa wahajiri hao akisisitiza kuwa, wahajiri Waafghani ambao hawajui la kufanya huko waliko kwenye kambi za wakimbizi nje ya nchi, wanaweza kurudi nchini Afghanistan.

Naye msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid, aliwahi kunukuliwa akisema: "tunayo taarifa kwamba wakimbizi Waafghani, wakiwemo walioko Qatar na Uturuki wanaishi katika hali mbaya; na hiyo ndiyo sababu ya sisi kuwazuia watu hao wasiondoke nchini".../