Mar 17, 2022 03:23 UTC
  • Dmitry Peskov
    Dmitry Peskov

Msemaji wa Rais wa Russia Dmitry Peskov ameyataja matamshi yaliyotolewa na Rais Joe Biden wa Marekani dhidi ya mwenzake wa Russia, Vladimir Putin kuwa "hayakubaliki" na "hayawezi kusamehewa."

Msemaji wa Rais wa Russia, Dmitry Peskov ameyasema hayo akijibu matamshi yaliyotolewa jana Jumatano na Joe Biden dhidi ya Vladimir Putin mbele ya waandishi wa habari mjini Washington. 

Ripoti zinasema kuwa, Joe Biden awali alijibu swali la mwandishi wa habari aliyeuliza kama yuko tayari kumwita Putin kuwa ni mhalifu wa kivita, akisema hapana; lakini muda mfupi baadaye alimtaka mwandishi huyo akariri swali lake, kisha akisema: "Nadhani Putin ni mhalifu wa vita."

Biden na Putin

Baada ya majibu hayo ya Biden televisheni ya CNN ya Marekani imetangaza kuwa: "hatua ya  Biden ya kutumia neno hilo inaonyesha mabadiliko katika msimamo wa hapo awali wa serikali ya Marekani."

Maafisa wa Marekani, akiwemo Joe Biden, hapo awali walikuwa wakijizuia kutumia maneno kama vile "uhalifu wa kivita" na "mhalifu wa kivita dhidi ya Russia na kiongozi wake" wakisisitiza kuwa kuna haja kwanza ya kufanyika uchunguzi.

Katika miezi kadhaa iliyopita Russia ililitahadharisha Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) kuhusu sera zake za kujipanua upande wa Mashariki na karibu mipaka ya nchi hiyo na kutoa mapendekezo ya dhamana na usalama kwa Marekani na NATO ambayo yamekataliwa. 

Russia imetangaza kuwa haina nia ya kuikalia kijeshi Ukraine na kwamba inakusudia kuipokonya silaha, kuiondoa katika mikono ya mafashisti na kizuia vita ya kimataifa. Vilevile Moscow inapinga sera za Shirika la Kijeshi la Nchi za  Magharibi NATO za kujipanua upande wa Mashariki hadi kwenye mipaka ya Russia.  

Tags