Apr 06, 2022 02:50 UTC
  • Marekani yakabiliwa na mgogoro wa madawa ya kulevya

Mgogoro wa madawa ya kulevya na vifo vinavyosababishwa na matumizi ya mihadarati nchini Marekani vinazidi kuongezeka.

Kiuo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (CDC) kimeripoti kuwa, watu 105,752 wameaga dunia nchini humo katika kipindi cha mwaka mmoja wa hadi mwezi Oktoba mwaka jana kutokana na kutumia kiasi kikubwa cha dawa za kulevya. 

Takwimu zinaonesha kuwa, vifo vinavyotokana na matumzi kupita kiasi ya dawa za kulevya vinaongezeka kwa kasi kubwa katika jamii ya Wamarekani weusi; taswira inayoonyesha kiwango jumla cha juu cha  vifo vya Wamarekakni weusi ikilinganishwa na raia wenzao  wazungu.  

Matumizi ya mihadarati yaongezeka kwa Wamarekani weusi 

Wakati huohuo, katika hotuba yake ya kila mwaka kuhusu hali ya jamii ya nchi hiyo, Rais Joe Biden wa Marekani amelitaja suala la utumiaji wa dawa za kulevya nchini humo kuwa ni tatizo linalohitaji hatua za haraka kukabiliana nalo. 

Tags