Aug 14, 2022 07:21 UTC
  • Kesi za kushambuliwa Waislamu nchini Austria zaongezeka

Jinai za kushambuliwa Waislamu kwa misingi ya dini yao zimeongezeka kwa kiwango cha kutisha nchini Austria.

Utafiti wa hivi karibuni unaonesha kuwa, asilimia 69 za kesi za kushambuliwa Waislamu katika nchi hiyo ya Ulaya ni hujuma dhidi ya wanawake wa Kiislamu, hususan wanaovaa Hijabu.

Ripoti ya utafiti wa mwezi Juni mwaka huu 2022 inaeleza kuwa, kesi zaidi ya elfu moja za jinai dhidi ya Waislamu kutokana na misimamo yao ya kidini ziliripotiwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Jumuiya ya Vijana wa Kiislamu ya Austria (MJÖ) hivi karibuni iliikosoa serikali ya nchi hiyo kwa kuchapisha kile ilichokiita "Ramani ya Uislamu", ambayo inaweka wazi maeneo ya misikiti na vyama vya Waislamu kote nchini humo.

Jumuiya ya Dini ya Kiislamu nchini Austria (IGGOE) pia imeonya dhidi ya kuwanyanyapaa Waislamu wanaoishi nchini humo na kusema hatua hiyo ni hatari kwa jamii na mfumo wa kidemokrasia nchini humo.

Maandamano ya kulaani chuki dhidi ya Uislamu Ulaya

Itakumbukwa kuwa, ripoti za mashambulio dhidi ya Waislamu nchini Austria zimeongezeka sana tangu shambulio la Vienna Novemba mwaka 2020. 

Kufuatia shambulio hilo, serikali ya Austria ilianzisha kile ilichokiita 'Operesheni Luxor' ambapo makazi na ofisi za Waislamu zilishambuliwa kwa lengo la kuzima eti 'Uislamu wa Kisiasa.'

Tags