Russia: Zelenskyy ni Bin Laden mwingine katika mavazi ya wazungu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i89704-russia_zelenskyy_ni_bin_laden_mwingine_katika_mavazi_ya_wazungu
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amemfananisha Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, na kiongozi aliyeangamizwa wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Oct 25, 2022 23:39 UTC
  • Maria Zakharova
    Maria Zakharova

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amemfananisha Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, na kiongozi aliyeangamizwa wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda.

Maria Zakharova, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, amesema katika mahojiano na kituo cha televisheni cha ya nchi hiyo, kwamba Volodymyr Zelenskyy, Rais wa Ukraine, ni Osama Bin Laden namba mbili kwa jamii ya kimataifa lakini katika sura na mavazi ya Kizungu.

Hapo awali, Volodin Vyacheslav, Spika wa Duma ya Russia, alimtaja Zelenskyy kuwa ni gaidi na kuliweka jina la rais huyo wa Ukraine katika orodha ya magaidi makubwa kama Osama bin Laden na magaidi wengine wa kimataifa, kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.

Volodymyr Zelenskyy

Kwa mujibu wa riwaya rasmi ya Ikulu ya Rais wa Marekani, White House, Osama bin Laden aliuawa Mei 2011 katika shambulio la askari wa vikosi maalumu cha nchi hiyo kwenye maficho yake huko Abbottabad, nchini Pakistan.

Tarehe 24 Februari 2022, Moscow ilianzisha opereseheni maalumu ya kijeshi dhidi ya serikali kibaraka ya Ukraine ili kuzuia nchi hiyo kujiunga na Jeshi la nchi za Magharibi la NATO na kuzuia Marekani na Ulaya kujiimarisha kijeshi katika mipaka ya Russia.