Serikali mpya ya Brazil kurejesha uhusiano wake wa kidiplomasia na Venezuela
(last modified Thu, 15 Dec 2022 07:09:29 GMT )
Dec 15, 2022 07:09 UTC
  • Serikali mpya ya Brazil kurejesha uhusiano wake wa kidiplomasia na Venezuela

Serikali mpya ya Brazil inapanga kurejesha uhusiano wa kidiplomasia wa nchi hiyo na Venezuela, ambao ulivunjwa wakati wa serikali iliyopita ya nchi hiyo.

Shirika la habari la Fars limeripoti kuwa, serikali ya  rais mchaguliwa wa Brazil Lula da Silva inapanga kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na Venezuela katika siku ya kwanza baada ya kuanza kazi rasmi.
Maur Vieira, chaguo la Da Silva kwa nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje amesema, mara tu atakapoapishwa Januari Mosi 2023, kiongozi huyo atatoa agizo la kuanzishwa uhusiano na Venezuela, ambao ulivunjwa enzi za utawala uliopita.
Vieira ameeleza kuwa mwanzoni mwa Januari, ujumbe maalumu wa kidiplomasia utatumwa Caracas kutafuta mahali utakapokuwepo ubalozi wa nchi hiyo kabla ya kuteuliwa balozi wa Brazil nchini Venezuela.
Rais mchaguliwa wa Brazil, Lula Da Silva wakati wa kampeni za uchaguzi

Mnamo 2020, serikali inayounga mkono Magharibi ya rais wa zamani wa Brazil, Jair Bolsonaro, iliwapiga marufuku viongozi wa serikali ya Venezuela kuingia nchini humo na kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Caracas.

Wakati wa uongozi wa Bolsonaro nchini Brazil, ambaye alikuwa akijitangaza kuwa mfuasi wa sera za rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump, aliitenga Brazil pamoja na shirika lake la taifa la mafuta Petrobras na Venezuela.
Tangu mwanzoni mwa 2019, serikali ya Marekani imeiwekea msururu wa vikwazo Venezuela ili kumlazimisha rais Nicolás Maduro wa nchi hiyo ajiuzulu.
Vikwazo vya Marekani vimelenga zaidi biashara ya mafuta ya Venezuela, inayochangia sehemu kubwa ya uchumi wa nchi hiyo.../
 

Tags