Rais wa Venezuela: Ubeberu wa Marekani umefikia kwenye hatua hatarishi zaidi
(last modified Mon, 26 Dec 2022 02:18:28 GMT )
Dec 26, 2022 02:18 UTC
  • Rais wa Venezuela: Ubeberu wa Marekani umefikia kwenye hatua hatarishi zaidi

Rais Nicolás Maduro wa Venezuela ametahadharisha kuwa ubeberu wa Marekani umeingia katika hatua hatarishi zaidi na unajaribu kufanya kila njia ili kuzusha mapigano na kuwasha moto wa vita duniani.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB, Maduro ametangaza kuwa ubeberu wa Marekani umeingia katika hatua ambayo sera, maadili, uchumi na jeshi la nchi hiyo viko katika hali mbaya, na kwa sababu hiyo Washington imekuwa hatari zaidi.

Rais wa Venezuela ameongezea kwa kusema, ubinadamu unahitaji kuingia katika hatua na awamu mpya ya ustawi, ushirikiano na mshikamano wa kimataifa.
Na hii ni katika hali ambayo, Marekani ingali inaendeleza sera zake za uhasama na uadui dhidi ya nchi zingine duniani.
Kwa mujibu wa rais Maduro, kwa miaka mingi, Marekani imekuwa ikijaribu kushadidisha satua na ushawishi wake katika nchi zingine duniani na kuziweka madarakani serikali na tawala vibaraka na tegemezi kwa nchi hiyo, lakini licha ya kutumia kila aina ya vitisho na sera za kiuadui, hadi sasa Washington imegonga mwamba katika njama zake hizo .../

 

Tags