Jan 10, 2023 07:52 UTC
  • Ubaguzi washadidisha mgogoro wa 'afya ya umma' Marekani

Miji na kaunti zaidi ya 200 nchini Marekani zimeutangaza ubaguzi wa rangi nchini humo kama mgogoro wa afya ya umma. Wataalamu wa afya wameonya kuwa, ubaguzi wa kimfumo wa miongo kadhaa umeendelea kuathiri afya za Wamarekani wasio wazungu.

Bodi ya Wasimamizi katika kaunti ya Orange jimboni California mwezi uliopita iliutangaza ubaguzi kuwa mgogoro wa afya ya umma, na kujiunga na mlolongo wa kaunti na miji ya Marekani iliyotoa tangazo hilo katika miaka ya karibuni.

Kaunti hiyo ilisajili ongezeko la visa vya ubaguzi wa rangi kwa asilimia 150 mwaka 2021, haswa ubaguzi wa rangi dhidi ya raia wa nchi hiyo wenye asili ya Asia na Visiwa vya Pacific.

Doug Chaffee, Mwenyekiti wa Bodi ya Wasimamizi katika kaunti ya Orange jimboni California anasema, "Kushuhudia ubaguzi kunahusishwa na ongezeko la kuwa katika hatari ya kupatwa na matatizo sugu ya kisaikolojia na ya kimwili, kama vile ugonjwa wa moyo, saratani, pumu, kisukari, kiharusi, Alzheimer (usahaulifu) na hata kujitoa uhai."

Baadhi ya miji ya US kama Cleveland, Las Vegas na Philadelphia ilitoa matangazo hayo dhidi ya ubaguzi wa rangi kufuatia mauaji ya kibaguzi na kutatanisha ya Mmarekani mweusi, George Floyd, Mei 2020, na pia kuwa wahanga wakubwa zaidi wa janga la Corona Wamarekani wenye asili ya Afrika kutokana na kunyimwa huduma na chanjo wakati huo.

Maandamano ya kupinga ubaguzi Marekani

Julai mwaka uliomalizika pia wa 2022, Matokeo ya utafiti uliofanywa katika majimbo mbalimbali ya Marekani yanaonyesha kuwa, vitendo na mienendo ya ubaguzi wa rangi dhidi ya raia wa nchi hiyo wenye asili ya Asia imeongezeka katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Mitazamo ya ubaguzi wa rangi na ya mrengo wa kulia ya baadhi ya vongozi na wanasiasa wa Marekani imechangia kushamiri ubaguzi wa rangi na vitendo vya ukatili vinavyosababishwa na chuki za ubaguzi nchini humo.

Tags