Jan 29, 2023 07:43 UTC
  • Rais Alberto Fernandez akiwa pamoja na  Olaf Scholz, Kansela wa Ujerumani
    Rais Alberto Fernandez akiwa pamoja na Olaf Scholz, Kansela wa Ujerumani

Rais wa Argentina amesema kuwa nchi za Amerika ya Latini, kinyume na nchi za Magharibi, hazina mpango wa kuipatia Ukraine silaha kwa kisingizio cha vita vinavyoendelea nchini humo.

Nchi za Ulaya na Magharibi kwa ujumla hasa Marekani  zimezidisha vikwazo  dhidi ya Shirikisho la Russia na zinaendelea kutuma aina mbalimbali za silaha nyepesi na nzito huko Ukraine na kuchochea moto wa vita nchini humo.  

Akizungumza na waandishi wa habari huko Buinos Aires akiwa na Olaf Scholz, Kansela wa Ujerumani, Rais Alberto Fernandez wa Argentina amesema kuwa: Argentina na nchi nyingine za Amerika ya Latini hazifikirii kutuma silaha huko Ukraine au katika eneo lolote lililoathiriwa na vita duniani kwa kisingizio cha kujiri vita nchini humo. 

Inapita zaidi ya miezi 11 sasa tokea kuanza vita huko Ukraine ambavyo vimekuwa na taathira kubwa mbaya za kisiasa, kiuchumi, kijeshi, kijamii na hata kiutamaduni huku nchi za Magharibi zikiendelea kutuma silaha na zana za kijeshi nchini humo.   

Russia imesema mara kadhaa kuwa hatua hiyo ya Wamagharibi kwa Ukraine itapelekea kuendeleau kwa mrefu hali ya mzozo na kuwa na athari zisizoweza kutabirika. 

Tags