Umoja wa Ulaya warefusha vikwazo kwa Russia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i9391-umoja_wa_ulaya_warefusha_vikwazo_kwa_russia
Baraza la Umoja wa Ulaya limerefusha vikwazo vya umoja huo dhidi ya Russia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 17, 2016 10:22 UTC
  • Umoja wa Ulaya warefusha vikwazo kwa Russia

Baraza la Umoja wa Ulaya limerefusha vikwazo vya umoja huo dhidi ya Russia.

Baraza la Umoja wa Ulaya limetangaza katika ripoti yake liliyotoa leo Ijumaa kuwa umoja huo umerefusha rasmi muda wa vikwazo lilivyoiwekea Russia mwaka 2014 baada ya kisiwa cha Crimea kutangaza kujitenga na Ukraine na kujiunga na Russia. Umoja wa Ulaya umechukua uamuzi huo katika kikao chake kilichohudhuriwa na wawakilishi wa nchi wanachama wa umoja huo. Vikwazo dhidi ya Russia vimerefushwa kwa muda wa mwaka mmoja yaani hadi kufikia tarehe 23 Juni mwaka kesho.

Vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Russia vinajumuisha marufuku ya uwekezaji vitega uchumi na uingizaji wa bidhaa kutoka kisiwa cha Crimea kuelekea Umoja wa Ulaya. Umoja wa Ulaya na Marekani mwaka 2014 ziliiwekea Russia vikwazo mbalimbali zikiituhumu Moscow kuwa inaingilia masuala ya ndani ya Ukraine, hatua ambayo imekabiliwa pia na radiamali ya Russia.