Mar 19, 2023 12:33 UTC
  • Atakayemkabidhisha askari wa Ukraine aliyeivunjia heshima Qur'ani kuzawadiwa $168,000

Rais Madan Kadyrov, wa eneo la Russia linalojiendeshea mambo yake la Chechnya ametenga zawadi ya ruble milioni 10 za Kirusi ambazo ni sawa na dola 168,000 za Kimarekani kwa atakayefanikisha kukamatwa akiwa hai, askari wa jeshi la Ukraine aliyeivunjia heshima Qur'ani tukufu kwa kuichoma moto nakala ya kitabu hicho kitakatifu.

Tovuti ya kituo cha habari cha Russia-Lyaum imeripoti kuwa, Kadyrov ametenga pia ruble milioni tano kwa mtu atakayeweza kuukabidhi mwili wa mwanajeshi huyo aliyeivunjia heshima Qur'ani tukufu.
Rais wa Chechnya ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa telegram: "sitatosheka na kulaani tu kitendo cha askari wa Ukraine, ambao hivi karibuni walizichoma moto kurasa za Qur'ani."
Kadyrov ameongezea kwa kusema: "mukiona kwenye ukurasa wangu wa telegram taswira za kitendo hiki kiovu, mujue kwamba, ninatangaza zawadi yenye thamani ya ruble milioni tano kwa ajili ya kuwaangamiza watu hawa; na mara mbili yake kwa kuwakamata wakiwa hai. Na tuzo hii ya fedha itabaki kama ilivyo bila kujali kama takwa hili litafanikishwa leo, kesho au hata mwaka ujao".
Rais Madan Kadyrov wa Chechnya

Rais wa Chechnya amemhutubu mwanajeshi huyo wa Ukraine kuwa ni mtu mwoga na kumwambia: "ewe uliyefunika uso wako kwa woga na hofu, fahamu kwamba popote utapokuwa umejificha utaadhibiwa tu; na nafsi yako iliyojaa woga katu haitapata amani na utulivu".

Wanajeshi kadhaa wa jeshi la Ukraine wenye misiamamo ya kufurutu mpaka wamefanya kitendo kiovu na cha kifidhuli kwa kusambaza kwenye mitandao ya kijamii video inayowaonyesha wakirarua na kuzichoma moto kurasa za nakala ya Qu'rani tukufu.
Wakati wakifanya kitendo hicho kiovu, askari hao wa jeshi la Ukraine wanaonekana pia wakitoa maneno ya matusi kuhusiana na Qur'ani, huku mmoja wao akisaga na kumimina shahamu ya nguruwe kwenye nakala hiyo ya Qur'ani Tukufu.../

 

Tags