Apr 03, 2023 09:51 UTC
  • Bolton: Trump ni saratani ya Chama cha Republican

Mshauri wa zamani wa Usalama wa Taifa wa Ikulu ya White House amemtaja Donald Trump, rais wa zamani wa Marekani, kuwa ni saratani ya Chama cha Republican.

John Bolton, Mshauri wa zamani wa Usalama wa Taifa wa Ikulu ya White House, ameonya kwamba ikiwa Trump ataondolewa hatiani au kesi yake itafutwa kwa sababu ya kutokamilika nyaraka za kisheria, atadai kuwa yuko na haki, na suala hili litampa dhamana ya kuteuliwa kuwa mgombea wa chama cha Republican katika uchaguzi wa rais mwaka 2024.

Bolton ameongeza kuwa: "Ninapaswa kuseme kwamba jibu la Trump baada ya kutangazwa kuwa na kesi ya uhalifu si jambo zuri kwa mustakabali wa chama na Trump ni saratani ya Chama cha Republican."

Bolton anaamini kwamba iwapo Trump atapatikana na hatia kabla ya uchaguzi wa mwaka ujao, Wamarekani wengi hawatataka mtu aliyepatikana na hatia awe rais wao.

Matamshi ya Bolton yametolewa baada ya Mahakama Kuu ya Manhattan mjini New York kumfungulia mashtaka rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kwa tuhuma za kulipa pesa za kiziba mdomo kwa mwanamke muigizaji wa filamu za ngono kuelekea uchaguzi wa rais wa mwaka 2016.

Trump atakuwa rais wa kwanza wa Marekani kushtakiwa kwa kosa la jinai kwa kulipa kiziba mdomo cha dola 130,000 kwa nyota wa filamu za ngono Stormy Daniels.

Trump na Stormy Daniels

Daniels, ambaye jina lake halisi ni Stephanie Clifford, alisema, alikuwa na uhusiano haramu wa kingono na Trump, ambaye ameoa.

Jumanne, Aprili 4, Trump amepangwa kufikishwa katika mahakama ya Manhattan, New York, kusomewa mashtaka yanayomkabili.

Tags