May 24, 2023 10:46 UTC
  • Uchunguzi wa maoni: Wapiga kura wa Marekani wana wasiwasi kuhusu maandalizi ya kiakili ya Biden na Trump

Kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni kuhusu uchaguzi uliofanyika karibuni nchini Marekani; wananchi wa nchi hiyo wanasema wana wasiwasi kuhusu kuwa tayari kiakili Rais wa sasa wa nchi hiyo Joe Biden na mtangulizi wake Donald Trump.

Uchaguzi wa rais nchini Marekani umepangwa kufanyika Novemba 5 mwaka kesho. Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, uchunguzi wa maoni uliofanywa na Taasisi ya Kitaaluma ya Uchambuzi wa Maoni Marist ya New York unaonyesha kuwa idadi kubwa ya wananchi wa Marekani wana wasiwasi kuhusu maandalizi ya kiakili na uwezo wa Rais wa sasa Joe Biden na Rais wa zamani Donald Trump wa kuiongoza nchi hiyo kama Rais.  

Kati ya asilimia 36 na 62 ya waliohojiwa katika uchunguzi huo wa maoni wamedhihirisha  wasiwasi kwa viwango tofauti kuhusu Biden kuwa tayari kakili kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake ya uongozi iwapo atashinda uchaguzi wa Rais mwaka kesho wa 2024. Wakati huo huo, uchunguzi huo wa maoni umeonyesha kuwa, hali ya Trump pia haitofautiani sana na ya Biden. 

Rais Joe Biden wa Marekani 

Asilimia 51 ya watu walioshiriki kwenye uchunguzi huo wa maoni nchini Marekani wanamini kuwa suala la kuwa tayari Trump kukalia kiti cha urais ni suala lenye kuibua wasiwasi mkubwa; huku asilimia 43 ya washiriki wakiwa na maoni tofauti.   

Joe Biden ambaye ana umri wa miaka 80 ndiye rais mzee zaidi katika historia ya Marekani. Amekuwa akishutumiwa mara nyingi na Warepublicans kwa kutowajibika ipasavyo mkabala wa majukumu yake kama Rais wa Marekani.

Tags