Uingereza yapiga kura kujiondoa Umoja wa Ulaya, EU
https://parstoday.ir/sw/news/world-i9814-uingereza_yapiga_kura_kujiondoa_umoja_wa_ulaya_eu
Matokeo yasiyo rasmi ya kura ya maoni iliyopigwa hapo jana kuhusu Uingereza kujitoa au kubakia ndani ya Umoja wa Ulaya (EU) yanaonyesha kuwa Waingereza wataondoka EU.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 23, 2016 22:28 UTC
  • Uingereza yapiga kura kujiondoa Umoja wa Ulaya, EU

Matokeo yasiyo rasmi ya kura ya maoni iliyopigwa hapo jana kuhusu Uingereza kujitoa au kubakia ndani ya Umoja wa Ulaya (EU) yanaonyesha kuwa Waingereza wataondoka EU.

Matokeo hayo yanaonyesha kumekuwepo na mchuano  mkali kati ya wanaotaka kubakia na wale wanaotaka Uingereza kujiondoa ndani ya Umoja huo wa Ulaya. Aidha ripoti zinaonyesha waliojitokeza kupiga kura hiyo ya maoni ni wengi ambapo asilimia 52 wamepiga kura ya kujiondoa EU huku 48 wakipiga kura ya kubakia. Sarafu ya Euro imepanda katika masoko ya fedha huku Paundi ya Uingereza ikiendelea kuporomoka na hivyo kuibua msukosuko katika masoko ya kifedha duniani.

Nigel Farage, wa chama cha upinzani cha  UK Independent Party ambaye anaongoza kampeni ya Uingereza kujiondoa EU amesema 'Juni 23 ni siku ya uhuru wa Uingereza.'

Imedokezwa kuwa chama cha upinzani cha Leba kimeanza kupanga hatua zitakazochukuliwa iwapo matokeo ya kura hiyo ya maoni ni Uingereza kujiondoa EU. Kiongozi cha chama cha LebaJeremy Corbyn anatathmini uwezekano wa kumtaka waziri mkuu David Cameron ajiuzulu kufuatia Uingereza kujiondoa EU huku baadhi wakisema Cameron atajiuzulu hata bila kushinikizwa.