Cameron ajiuzulu kama Waziri Mkuu baada ya Uingereza kujiondoa EU
https://parstoday.ir/sw/news/world-i9850-cameron_ajiuzulu_kama_waziri_mkuu_baada_ya_uingereza_kujiondoa_eu
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amejiuzulu baada ya Waingereza kupiga kura ya kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 24, 2016 03:53 UTC
  • Cameron ajiuzulu kama Waziri Mkuu baada ya Uingereza kujiondoa EU

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amejiuzulu baada ya Waingereza kupiga kura ya kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.

Baada ya wale waliokuwa wakiunga mkono kujiondoa EU kupata asilimia 52 ya kura, Cameron amelihutubia taifa nje ya ofisi yake na kutangaza uamuzi wake wa kujiuzulu. Cameron atabakia madarakani hadi mwezi Oktoba wakati atakapokabidhi hatamu za uongozi kwa waziri mkuu mpya atakayechaguliwa katika kongamano la chama tawala cha Conservative. Amesema mazungumzo ya kujiondoa EU yanapaswa kufanyika chini ya uongozi mpya.

Hatua ya Uingereza kujiondoa EU imepelekea Pauni kuporomoka huku masoko ya fedha duniani yakikumbwa na msukosuko.

Wakati huo huo hatua ya Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya inatazamiwa kupelekea mataifa mengine ya umoja huo kuanzisha mikakati ya kuondoka na hivyo kupelekea kuanza kusambaratika umoja huo.

Nigel Farage, wa chama cha upinzani cha UK Independent Party ambaye anaongoza kampeni ya Uingereza kujiondoa EU amesema 'Juni 23 ni siku ya uhuru wa Uingereza.'